Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, maandamano makubwa yalifanyika katika maeneo mbalimbali duniani kote kwa mnasaba wa Siku ya Wafungwa wa Kipalestina. Maandamano haya yanafanyika katika hali ambayo hasira ya umma imeongezeka kutokana na ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na wavamizi wa Kizayuni dhidi ya wafungwa, hususan kupitishwa kwa sheria inayoruhusu utekelezaji wa hukumu ya kifo.
Maandamano pia yalifanyika maeneo ya West Bank, ambapo makundi ya waandamanaji yalianza matembezi yao kutoka jengo la baraza la manispaa katika mji wa Nablus kuelekea Uwanja wa Mashahidi katikati ya mji huo, na ikashuhudiwa ushiriki mkubwa wa wakazi pamoja na taasisi rasmi na za wananchi.
Morocco, Australia na Tunisia zilikuwa miongoni mwa nchi zilizoongoza maandamano haya. Nchini Morocco, maelfu ya waandamanaji walielekea bungeni katika mji mkuu na kupaza sauti dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na wavamizi wa Kizayuni ndani ya magereza, wakitaka kufutwa kwa sheria za kidhalimu nchini Israel na kuonesha uungaji mkono wao kwa wafungwa.
Nchini Australia pia, mji wa Melbourne ulishuhudia maandamano makubwa, ambapo waandamanaji walibeba mabango yenye kauli mbiu za kuiunga mkono Palestina na kudai hatua za kimataifa ili kuhakikisha kuachiwa huru kwa wafungwa na kufutwa kwa sheria ya adhabu ya kifo.
Zaidi ya wafungwa 9,600 wa Kipalestina, wakiwemo watoto na wanawake, wanashikiliwa katika magereza ya wavamizi wa Kizayuni, ambapo wanakabiliwa na mateso, njaa na kupuuzwa kiafya, hali ambayo kwa namna ya kikatili imesababisha kufariki mishahidi makumi ya wafungwa hao.
Chanzo: iumsonline.org
Maoni yako