Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, maandishi kamili ya ujumbe wa Ayatollah A‘rafi, mkuu wa hawza Iran, katika kujibu juhudi za kukata tamaa za Trump mhalifu na maadui wengine walioshindwa za kuleta mgawanyiko kati ya watu na viongozi wa Iran ni kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu, na rehma na amani zimshukie Muhammad na Ahlul-Bayt wake watoharifu
إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ یَنْصُرْکُمْ وَیُثَبِّتْ أَقْدَامَکُمْ
Mlolongo wa jumbe, twiti na misimamo ya kishetani ya Trump, kwa upande mmoja imetokana na hila na chuki ya kishetani dhidi ya haki, uadilifu, uhuru, heshima ya mwanadamu na hotuba ya mbele ya Mapinduzi ya Kiislamu; na kwa upande mwingine inaonesha undani wa kishetani wa nafsi yake na ni kioo cha utamaduni na roho ya ustaarabu wa kibeberu na ukatili wa kinyama; na juu ya yote hayo, inaashiria machafuko ya nafsi, kukata tamaa katika uwanja wa mapambano, na kushindwa katika kukabiliana na fikra za kimataifa na za umma na pia na kambi ya Iran ya Kiislamu na muqawama wenye heshima. Kina cha tofauti, mtawanyiko na nyufa kubwa ndani ya jamii ya Marekani na taasisi zake rasmi, na pia ndani ya serikali na vyama vyake, pamoja na machafuko katika misimamo ya marafiki na washirika wa Marekani ndani ya Ulaya na dunia, vimesababisha mkanganyiko kwa Marekani na Wazayuni; na mshikamano wa mataifa ya eneo na dunia dhidi ya vita, uvamizi, ukatili na umwagaji damu, pamoja na uimara na ustahimilivu wa Iran na mhimili wa muqawama, umeongeza taharuki na machafuko katika kambi ya Marekani na Wazayuni.
Machafuko haya, uzushi na maneno ya kipuuzi ya hivi karibuni na yanayoendelea ya Trump yametokana na kushindwa huku kimkakati na hali ya kukata tamaa ya uwanjani, na kamwe hayatavuruga safu imara kama chuma ya taifa kubwa la Iran, vikosi vyake vya kijeshi na viongozi wake.
Watu wote duniani wajue kwamba; sasa nyoyo, hatua na safu za taifa la Iran na muqawama, pamoja na taasisi zote, viongozi, vyombo na mikondo ya Iran ya Kiislamu na muqawama, zimeungana zaidi na kushikamana zaidi, na ziko tayari zaidi kwa kukabiliana na njama na hila za adui; na kwa mshikamano na umoja, pamoja na kumfuata kiongozi mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu (daima baraka zake zidumu), watatembea katika njia ya kulinda heshima, utu na sharafu yao.
Taasisi ya dini, wanazuoni wakubwa wa dini, hawza za kielimu, vyombo na taasisi za hawza na za kielimu, pamoja na wanahawza wote, kwa kufuata Imam muasisi (r.a) na kiongozi mpendwa na shahidi (r.a) na maraji‘ wakubwa wa taqlid (baraka zao zidumu), wako thabiti katika ahadi yao katika njia ya uhuru na heshima ya Iran, na katika mkondo wa malengo ya Uislamu, Mapinduzi na mashahidi watukufu; na kwa sauti kubwa wanasisitiza umoja miongoni mwao, mshikamano na taifa la Iran, kufuata uongozi mtukufu na uamiri mkuu wa majeshi, na kushirikiana na vikosi vya kijeshi na mhimili wa muqawama; na wanayaona maneno ya kipuuzi na ya kubuni ya Trump ya kujaribu kuunda taswira ya mgawanyiko na tofauti na nyufa katika safu za taifa na viongozi waheshimiwa kuwa ni batili na yasiyo na thamani, na wanayalaani.
Nauombea Uislamu ushindi na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yenye heshima pamoja na mhimili wa muqawama kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kwa uangalizi wa Imam Wali al-‘Asr (a.f).
Alireza A‘rafi
Mkuu wa Hawza nchini Iran
Maoni yako