Jumatano 22 Aprili 2026 - 02:15
Umuhimu wa kuimarisha vyombo vya habari vya haki mbele ya mashambulizi ya propaganda dhidi ya Iran/ Vita vya vyombo vya habari ni uwanja mkuu wa mapambano kati ya haki na batili katika zama za leo

Hawza/ Sheikh Mahdi al-Sumaida'i, Mufti wa Iraq, katika kikao cha “Mustakbali wa Mapambano” alisisitiza umuhimu wa kuimarisha vyombo vya habari vya kambi ya haki, na akavielezea vita vya vyombo vya habari kuwa ndio uwanja mkuu wa mapambano kati ya haki na batili katika zama za sasa. Aidha alikosoa upotoshaji mkubwa wa ukweli kuhusu Iran, Ghaza, Lebanon, Yemen na Iraq unaofanywa na baadhi ya vyombo vya habari vya Kiarabu na Magharibi.

Kwa mujibu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, katika kikao cha “Mustakbali wa Mapambano” kilichofanyika siku ya Jumapili kwa juhudi za Majma ya Qadimun, Sheikh Mahdi al-Sumaida'i alirejea nafasi yenye uzito ya vyombo vya habari katika historia na kusema: Tangia zama za kale hadi leo, kumekuwa na mikondo miwili—“haki” na “batili”—ambayo imekuwa katika mapambano ndani ya uwanja wa vyombo vya habari; mkondo wa batili, kwa kutumia uongo na kupotosha ukweli, umejaribu kupotosha fikra za umma na kuzuia kudhihirika kwa ukweli.

Sheikh al-Sumaida'i, huku akikosoa ubora wa vyombo vya habari vya mkondo wa batili, alibainisha kuwa: Moja ya changamoto kuu za leo ni udhaifu na uzembe wa vyombo vya habari vya kambi ya haki; huku maadui wakitengeneza simulizi za uongo kwa wingi na kuathiri fikra za umma, vyombo vya habari vya haki vinapaswa kuwa na uwepo hai zaidi na wenye athari kubwa.

Alisisitiza umuhimu wa kutumia zana za kisasa za mawasiliano, kwa kusema: Leo, mitandao ya kijamii, vyombo vya habari vya kidijitali na nyenzo mbalimbali za mawasiliano vinatoa fursa muhimu ya kuwasilisha ukweli, na ni lazima wanaharakati wa kambi ya haki watumie uwezo huu ipasavyo.

Mufti wa Iraq aliendelea kwa kurejea matukio ya eneo hili, akasema: Katika vita vya hivi karibuni katika eneo, ikiwa ni pamoja na Ghaza, Lebanon, Iraq, Yemen na pia kuhusiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, tumeshuhudia upotoshaji mkubwa wa ukweli kutoka kwa baadhi ya vyombo vya habari vya Kiarabu na Magharibi; kiasi kwamba wakati mwingine mnyanyasaji huoneshwa kama mhanga na mhanga huonyeshwa kama mnyanyasaji.

Alisisitiza kuwa: Katika hali kama hizi, kunyamaza mbele ya kupotoshwa kwa ukweli hakukubaliki, na ni wajibu kwa watu wote wa haki kusema ukweli kwa ujasiri na uwazi, na kutoruhusu simulizi zisizo sahihi kutawala fikra za umma.

Mwisho, Sheikh al-Sumaida'i, kwa kutoa wito wa kuimarishwa kwa “vyombo vya habari vya kambi ya haki”, alisema: Kusema ukweli si tu wajibu wa kidini, bali pia ni jambo la msingi katika kuisaidia haki na kupambana na batili, na linaweza kubadilisha mwelekeo wa matukio ya baadaye.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha