Jumanne 14 Aprili 2026 - 13:30
Ukatili mkubwa wa Waisraeli kusini mwa Lebanon waacha idadi kubwa zaidi ya mashahidi na majeruhi

Hawza/ Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea na mashambulizi yake ya kinyama na yaliyopangwa dhidi ya kusini mwa Lebanon.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha trjama cha Shirika la Habari la Hawza, utawala wa Israel unaendeleza mashambulizi yake ya kinyama na yaliyopangwa dhidi ya kusini mwa Lebanon; mashambulizi ambayo kila mara yanapokumbana na maumivu na kushindwa katika uwanja wa vita mbele ya utetezi wa wapiganaji jasiri wa muqawama, huzidi kuwa makali na kuelekezwa kwa kiwango cha juu zaidi cha ukatili na tabia za uvamizi. Katika maendeleo mapya, ndege za kivita za adui Muisraeli zililenga kituo cha “Shirika la Afya la Kiislamu” katika mji wa Sayr al-Gharbiyah katika mji wa Nabatiyah kusini, na pia ulishambulia kwa mabomu mji wa Nabatiyah al-Fawqa katika eneo hilo hilo.

Ndege za kivita za adui Muisraeli zilifanya mashambulizi mawili ya anga dhidi ya mji wa Mifdoun maeneo ya Nabatiyah na mji wa al-Bazuriyah katika mji wa Sur. Wakati huohuo, mashambulizi mawili ya Israel pia yalilenga nyumba za “al-Siyad” na “Majdal Zoun” katika mji huo huo. Vilevile mashambulizi mawili ya anga ya adui yalitekelezwa katika maeneo ya pembezoni mwa mji wa Shuqin kusini mwa Lebanon.

Mashambulizi mazito ya mizinga ya utawala wa Kizayuni yalifikia katika miji ya al-Haniyah, al-Qalilah na al-Mansuri; huku ndege za kivita za Israel zikishambulia kwa mabomu mji wa Siddiqin katika mji wa Sur. Mizinga ya adui pia ililenga mji wa Bint Jbeil na miji ya Kounin na Qabrikha, na ndege za kivita pia zilishambulia mji wa al-Khiyam.

Mashambulizi haya ya Israel yalisababisha kuuawa kwa watu watatu katika kila moja ya maeneo ya al-Bazuriyah, al-Nabatiyah al-Fawqa na Sayr al-Gharbiyah. Wakati huohuo Wizara ya Afya ya Lebanon ilitangaza kwamba, kutokana na shambulio la anga la adui Muisraeli dhidi ya mji wa Tafahata, watu 9 waliuawa kishahidi na 13 kujeruhiwa.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa

Katika muendelezo wa matukio, Vikosi vya Muda vya Umoja wa Mataifa nchini Lebanon “UNIFIL” juzi (Jumapili) vilirekodi na kuweka kumbukumbu ya mfululizo wa mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la uvamizi la Israel dhidi ya vikosi na magari yake. Kikosi hicho kilitangaza kwamba, kuna matukio mawili yaliyorekodiwa ambapo wanajeshi wa adui walitumia tanki la “Merkava” kugonga na kuharibu magari ya Umoja wa Mataifa.

“UNIFIL” ilieleza kwamba; moja ya matukio hayo ilisababisha uharibifu mkubwa kwa magari ya shirika hilo. Pia wanajeshi wa uvamizi walifunga barabara ya “al-Bayyadah”; barabara ambayo ni njia muhimu ya kufikia makao makuu na maeneo ya kikosi hicho. UNIFIL pia ilitaja kurushwa kwa risasi ambazo ziligonga magari ya Umoja wa Mataifa na kusababisha hasara; moja ya risasi hizo ilipita umbali wa mita moja tu kutoka kwa mmoja wa walinda amani.

Katika mwendelezo wa mvutano wa uwanjani, ripoti zilionyesha kwamba; wanajeshi wa uvamizi wameharibu kamera za ulinzi katika makao makuu ya “UNIFIL” huko al-Naqoura na pia katika maeneo mengine matano kando ya Mstari wa Bluu kuanzia Ras al-Naqoura hadi Maroun al-Ras.

Vikosi vya uvamizi, siku ya Jumamosi iliyopita pia vilipaka rangi kwenye madirisha ya lango la makao makuu ili kuzuia uoni wa mazingira ya nje; hatua iliyochukuliwa kwa lengo la kuzuia shughuli za ufuatiliaji na uwekaji kumbukumbu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha