Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, ujumbe wa Ayatullah Maka'rem Shira'zi ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.
Taifa tukufu la Iran na wapenzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, Baraza la wataalamu wa Uongozi katika kipindi kigumu tunachopitia wamechukua maamuzi kwa kutimiza wadhifa wao wa kisheria na kikatiba.
Baraza hili baada ya kufanya utafiti kwa shakhsia mbalimbali wamemchagua Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei (mola amuhifadhi) kuwa ni Kiongozi wa tatu wa Mapinduzi ya Kiislamu na wametimiza hoja kwa watu wote.
Kwa sasa ni lazima Wananchi na nguzo za utawala, kwa kukubaliana na uteuzi huu bora, wataiendeleza njia ya Mapinduzi iliyojaa nuru na kuendeleza umoja na uthabiti mpaka ushindi wa mwisho utakapo patikana.
Nikiwa natoa salamu zangu za rambirambi kwa mara nyengine kutokana na shahada ya Kiongozi wa Mapinduzi, Majenerali wa jeshi, wananchi watukufu wa Iran, watoto na wanawake wenye kudhulumiwa, ninaupongeza uteuzi huu, na ninamuomba Mola aipe Iran ushindi na awadhalilishe maadui.
Na amani iwe juu yenu na rehma za Mwenyezi Mungu na Baraka zake
Qum, Na'sir Maka'rim Shi'ra'zi
18 isfand 1404 - 9 march 2026.
Maoni yako