Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Katika ujumbe wa Sheikh Naim Qassim Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanoni imekuja hivi:
Shahada tukufu ya Kiongozi na Walii wa mambo, mtukufu Sayyid Ali Khamenei (r.a) ambayo ni alama kubwa ya utukufu, ikhlasi, muqawama na kujitolea katika njia ya Mwenyezi Mungu - alama ya Shahada katika njia ya Bwana wa Mashahidi, Imam Hussein (as) -. Natoa salamu za rambirambi kwa Mtukufu Imam wa zama (aj), umma wa Kiislamu, watu wote wanaotaka kuwa huru duniani na Taifa adhimu la Iran.
Sheikh Naim Qassim aliongeza kusema: Kwa Moyo wenye kujaa uchungu na huzuni ninamkumbuka Mtukufu Imam Sayyid Ali Khamenei (ra), mwanazuoni wa Kiungu na Kiongozi wa kiungu, na vilevile ninahisi fakhari na utukufu kwa sababu Kiongozi wa umma wa Kiislamu na walii wa jambo la umma huu, amepata shahada katika Mwezi mtukufu zaidi na siku bora zaidi. Yeye ndie ameiongoza njia ya jihadi na muqawama, dhidi ya madhalimu na majabari Wakimarekani na Kiisraeli pamoja na maadui wa dini na ubinadamu, mpaka kupata daraja hili, uhai wake mtukufu ameumaliza kwa kupata shahada.
Maoni yako