Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Mohamed Muizzu, Rais wa Maldives, aliwapongeza wananchi wa Maldives pamoja na Umma wa Kiislamu kwa kuwadia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Alisisitiza umuhimu wa kuzingatia faradhi, adabu, hukumu, sheria na kanuni za mwezi huu nchini Maldives, na akasema kuwa kuijenga jamii inayoswali mara tano kwa siku, inayowalea vyema watoto na vijana wake, na inayowaheshimu wakubwa wake, ndio msingi wa maadili na utawala bora kwa taifa.
Aidha, aliielezea jamii bora kuwa ni ile isiyo tumia dawa za kulevya na mazoea mabaya, inayofuata misingi ya Kiislamu na maadili ya kitamaduni.
Dkt. Mohamed Muizzu aliongeza kuwa; serikali inaunga mkono aina yoyote ya shughuli zinazoendeleza maadili na tunu za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Pia alisisitiza kuwa mikusanyiko ya kijamii na kifamilia kama vile futari na daku huchangia kuimarisha mahusiano ya kijamii, huruma na mapenzi ndani ya mwezi wa Ramadhani.
Chanzo: PSM News
Maoni yako