Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, maandamano hayo yalifanyika kwa lengo la kumuunga mkono Ayatollah Sayyid Ali Khamenei na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, pamoja na kulaani vikali tukio la kigaidi lililotokea katika Msikiti wa Khadijah al-Kubra mjini Islamabad.
Katika hafla hiyo, wanazuoni walitaka kukamatwa mara moja kwa wahusika na wanaowaunga mkono katika kitendo hicho cha kigaidi na waadhibiwe kwa mujibu wa sheria. Pia walisisitiza umuhimu wa kufanyika kwa uchunguzi wa wazi na kutangazwa kwa matokeo yake kwa umma, wakieleza kuwa, kudhibiti wimbi la ugaidi ni miongoni mwa majukumu muhimu ya taasisi za usalama na serikali.
Onyo kuhusu vitisho vya Marekani dhidi ya Kiongozi Mkuu
Katika maandamano hayo, Hujjatul-Islam Sayyid Hasan Zafar Naqvi, Katibu Mkuu wa Majlis Wahdat Muslimeen Pakistan, alilaani vitisho vya Rais wa Marekani dhidi ya Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na kuvieleza kuwa, ni hatua hatari kwa usalama wa eneo. Alisisitiza kuwa; Ayatollah Sayyid Ali Khamenei ni alama ya umoja na mapambano ya ulimwengu wa Kiislamu, na kwamba hatua yoyote ya uhasama dhidi yake inaweza kuwa na athari kubwa za kikanda.
Wanazuoni wa Pakistan waliongeza kuwa, Iran na Pakistan ni nchi mbili za Kiislamu ndugu zenye uhusiano wa kihistoria, kidini na kimkakati, na kwamba hatua yoyote dhidi ya Iran itachukuliwa kuwa tishio kwa utulivu wa eneo.
Msisitizo juu ya umoja wa kitaifa na kupambana na ukosefu wa usalama
Wazungumzaji pia walieleza kuwa; kuna juhudi za baadhi ya madola ya kimataifa za kuleta machafuko katika eneo, hivyo wakasisitiza umuhimu wa umoja wa kitaifa na kuweka mkakati wa pamoja wa kupambana na ugaidi. Waliongeza kuwa, Pakistan haiwezi kuvumilia tena ukosefu wa usalama, na taasisi husika zinapaswa kutekeleza majukumu yao ya kisheria.
Wawakilishi wa dini nyingine pia walihudhuria hafla hiyo; Manoj Chauhan kutoka jamii ya Kihindu na Pastor Rahmat Lal kutoka jamii ya Kikristo walitoa pole kwa mashahidi wa tukio la msikiti wa Waislamu wa Kishia mjini Islamabad na kusisitiza mshikamano wa kitaifa.
Msisitizo juu ya sera ya nje na uungaji mkono kwa Palestina
Katika sehemu nyingine ya hotuba zao, washiriki walisisitiza umuhimu wa kupitia upya sera ya nje ya Pakistan kwa kuzingatia maslahi ya taifa na manufaa ya Umma wa Kiislamu, na wakatangaza tena mshikamano wao na watu wa Palestina.
Maoni yako