Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ghazi Hanina, Rais wa Baraza la Wadhamini wa Muungano wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon, katika ujumbe wa video kwa mnasaba wa kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, alisisitiza juu ya upeo wa kimataifa na malengo ya kiummati ya mapinduzi haya.
Tarjama ya maandishi ya ujumbe wake ni kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
Mara tu ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ulipotangazwa kwa jina la Kiislamu na kupewa sifa ya Kiislamu kwa jamhuri ya Iran chini ya jina la “Jamhuri ya Kiislamu ya Iran”, jambo hili lenyewe ni uthibitisho kwamba mapinduzi haya makubwa na yenye baraka, yaliyoongozwa na Imam Ruhullah Khomeini (rahmatullahi alayh), ni mapinduzi kwa ajili ya Uislamu na Waislamu.
Na hili ndilo pia lililosisitizwa katika Katiba ya Iran; miongoni mwa mambo hayo ni kuiunga mkono Palestina, kuwatetea wanyonge (mustadh‘afin), na kusisitiza mwelekeo wa umoja. Haya yote ni uthibitisho kwamba Mapinduzi haya ya Kiislamu yaliyopata ushindi tarehe 22 Bahman, sawa na tarehe 11 Februari, ni mapinduzi ya Kiislamu kwa mataifa yote ya ulimwengu wa Kiislamu na watu wote wanaodhulumiwa duniani.
Maoni yako