Jumatano 11 Februari 2026 - 01:30
Vyombo vya habari ndivyo vinavyojenga na kuitambulisha jamii/ Jihadi ya ubainishaji ni ulazima usiopingika katika zama za vyombo vya habari

Hawza/ Mjumbe wa Baraza la Utambuzi wa Maslahi ya Mfumo (Majmaʿ Tashkhis-e Maslahat-e Nezam) akisisitiza nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga utambulisho wa kijamii, alisema: Iwapo mafundisho ya Uislamu, uhalali wa Mapinduzi ya Kiislamu na fikra za juu za Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi zitawasilishwa ipasavyo kwa ulimwengu kwa lugha ya vyombo vya habari, dunia itainama mbele ya utamaduni na ustaarabu huu.

Kwa mujibu Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Mohsen Araki, mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza za Kielimu, katika mahojiano na mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza mjini Mashhad, akielezea kwamba kila jamii ina utambulisho wake maalumu, alisema: kwa mujibu wa kaida ya “Watu wako juu ya dini ya watawala wao” (الناس علی دین ملوکهم), utambulisho wa kijamii wa kila jamii huundwa na watawala wake, na zana za utawala huwa na nafasi kuu katika kuunda utambulisho huo.

Vyombo vya habari; chombo kikuu cha kujenga utambulisho wa tawala

Akizungumzia nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga fikra za umma, aliongeza kuwa; zana za watawala za kujenga utambulisho ni njia za kupokea maudhui. Kupitia njia hiyo, vyombo vya habari husambaza dhana zinazotengeneza utambulisho wa watu, wakati mwingine hata bila watu wenyewe kuwa na uchaguzi wa makusudi katika mchakato huo.

Ayatullah Araki akirejea mabadiliko ya kihistoria mwanzoni wa Uislamu alisema: tunaishuhudia jamii ya zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ambayo Qur’ani inaielezea kuwa “umma bora”, lakini baada ya muda mfupi jamii hiyo hiyo inageuka na kufikia janga la Karbala. Sababu ya mabadiliko hayo ilikuwa kubadilika kwa utawala na matumizi tofauti ya nyenzo za mawasiliano.

Aliendelea kusema kuwa; katika zama hizo, nyenzo za mawasiliano za tawala zilikuwa khutba za Ijumaa, mashairi na njia rahisi za mawasiliano, lakini hata nyenzo hizo ziliweza kubadilisha jamii kwa kiasi kikubwa.

Jihadi ya ubainishaji; wajibu wa kimkakati katika enzi ya vyombo vya habari

Mjumbe huyo wa Baraza la kutambulisha Maslahi ya Mfumo huku akisisitiza uwezo wa vyombo vya habari vya leo alisema: ikiwa leo tunaweza — na bila shaka tunaweza — kuwasilisha mafundisho ya Uislamu, uhalali wa Mapinduzi ya Kiislamu na fikra za Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kwenye ulimwengu, dunia itakubali fikra, ustaarabu na utamaduni wetu.

Akirejea msisitizo wa mara kwa mara wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, aliongeza kusema: wajibu wetu ni jihadi ya ubainishaji, jihadi ambayo inapaswa kufuatiliwa kwa umakini na kwa busara.

Ayatullah Araki huku akifafanua dhana ya vyombo vya habari alisema: vyombo vya habari si tu znyenzo zinazojulikana leo; wakati mwingine wazo la kielimu lisipowasilishwa kwa kuzingatia hadhira, linaweza lisieleweke au likasababisha kutoelewana. Hivyo, katika kuwasilisha dhana, ni lazima kuzingatia maudhui yanayolingana na hadhira, kuelewa lugha ya hadhira, na kutumia mtindo mzuri na wa kisanaa katika uwasilishaji.

Alitaja nguzo tatu kuu za kazi ya vyombo vya habari kuwa ni:

1. Uimara na uzito wa maudhui,
2. Ulinganifu wa maudhui na hadhira,
3. Uzuri wa mtindo wa uwasilishaji.

Alisema kuwa; nguzo hizi ndio msingi wa kazi ya vyombo vya habari yenye mafanikio, na zote zinahusiana na fasihi na uwasilishaji, kama ambavyo Qur’ani Tukufu pia imetumia viwango vya juu vya fasihi.

Mwisho, Ayatullah Araki aliwashukuru waandaaji wa Tamasha la Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii “Salman”, akisema: Ni matumaini yetu kwa Mwenyezi Mungu, awasaidie wale walioanzisha mkutano huu muhimu, na kwamba hatua hii iwe mchango mkubwa katika kuboresha shughuli za vyombo vya habari na kuinua uzalishaji wa maudhui ya habari nchini.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha