Jumatano 11 Februari 2026 - 01:00
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameafiki kutolewa msamaha, kupunguza au kubadilisha adhabu kwa zaidi ya watu elfu mbili waliotiwa hatiani

Hawza/ Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amekubali ombi la Mkuu wa Idara ya Mahakama kuhusu kutoa msamaha, kupunguza au kubadilisha adhabu kwa watu elfu mbili mia moja na nane (2108) waliotiwa hatiani na mahakama za kawaida na za Mapinduzi, Mahakama ya Vikosi vya Kijeshi, pamoja na taasisi ya adhabu za kiserikali (Taʿzirat-e Hokumati).

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Mohseni Eje’i, katika barua aliyomwandikia Ayatullah Khamenei kutokana na mnasaba wa sikukuu za mwezi wa Shaban na maadhimisho ya miaka arobaini na saba ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, alikuwa ameomba msamaha, kupunguzwa au kubadilishwa adhabu za wafungwa hao.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha