Jumamosi 7 Februari 2026 - 09:00
Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni matumaini na uimara kwa wanyonge duniani

Hawza/ Baraza la Mashia nchini India, katika ujumbe wake limesisitiza kuwa; Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran si tu alama ya uhuru na kujitawala kwa taifa la Iran, bali pia ni mjumbe wa matumaini, ustahimilivu na mapambano dhidi ya dhuluma na uonevu kwa wanyonge na wanaotafuta haki duniani kote.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Baraza la Mashia India, katika ujumbe wake limesisitiza kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran si tu alama ya uhuru na kujitawala kwa taifa la Iran, bali pia ni mjumbe wa matumaini, ustahimilivu na mapambano dhidi ya dhuluma na uonevu kwa wanyonge na wanaotafuta haki duniani kote. Baraza hili katika ujumbe wake limechukulia ustahimilivu na kusimama imara kwa taifa la Iran mbele ya mashinikizo, njama na vikwazo vya kidhalimu kuwa ni ishara wazi ya nguvu ya haki na uadilifu, na limepongeza nafasi ya uongozi wa uelekezi na wa hekima wa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika kulinda mapinduzi na kuliongoza taifa kuielekea heshima, utulivu na kujiamini.

Matini ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

“Na wakapanga njama, na Mwenyezi Mungu akapanga, na Mwenyezi Mungu ndiye Mbora wa wanaopanga.”

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni matokeo ya mapinduzi makubwa ya wananchi na ya Kiislamu yaliyozaa kwa imani, utambuzi, uhuru na kusimama dhidi ya dhuluma na uonevu. Mapinduzi haya si tu alama ya uhuru na kujitawala kwa taifa la Iran, bali pia yana ujumbe wa matumaini na mapambano kwa wanyonge na wanaotafuta haki duniani. Kusimama imara kwa Iran mbele ya mashinikizo, njama na vikwazo vya kidhalimu ni ushahidi wazi kwamba mfumo unaotegemea haki na uadilifu hauwezi kamwe kushindwa.

Katika njia hii, nafasi ya uongozi wa uelekezi, wa hekima unaotoa mwamko wa utambuzi wa Kiongozi Mkuu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei (Mwenyezi Mungu aendelee kumlinda), imekuwa ya msingi na isiyoweza kufananishwa. Uongozi wake sio tu umelinda Mapinduzi ya Kiislamu dhidi ya fitina na hila za ndani na nje, bali pia umeliongoza taifa la Iran mbele kwa heshima, utulivu na kujiamini.

Kwa upande mwingine, sera za uingiliaji na ukoloni za Marekani, dhuluma na mashambulizi endelevu ya utawala wa Kizayuni, na uungwaji mkono kipofu na baadhi ya nchi za Ulaya, vinahesabiwa kuwa tishio kubwa kwa amani ya dunia. Vikwazo vya kidhalimu, madai ya uongo ya haki za binadamu na viwango vya pande mbili, kwa hakika ni pigo kwa dhamiri ya dunia. Baraza la Mashia wa India, huku likitangaza chuki kali, hasira na wasiwasi wake, linapinga sera hizi za kikoloni na zisizo za kibinadamu.

Sisi kwa yakini kamili tunatangaza kuwa  njia ya mapambano uhuru na kusimama katika haki haitasimamishwa kamwe kwa mashinikizo, vitisho na vikwazo. Taifa la Iran chini ya uongozi wa kiongozi wake mwenye hekima, kama zamani, litasonga mbele kwa fahari na ustahimilivu.

Na amani iwe juu ya anayefuata uongofu.

Baraza la Mashia nchini India.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha