Alhamisi 22 Januari 2026 - 23:30
Utetezi thabiti wa Maraji juu ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Iran

Hawza/ Mtukufu Ayatullah Makarem Shirazi amesisitiza: Kila mtu au utawala wowote utakaomtishia Kiongozi wa Mapinduzi na marjaiya (uongozi wa kidini), au—Mungu apishe mbali—ukajaribu kuwadhuru, kwa lengo la kuupiga pigo Umma wa Kiislamu na mamlaka yake, una hukumu ya “muharib” (mtu anae upiga vita Uislamu), na aina yoyote ya ushirikiano au kuutia nguvu utawala huo na Waislamu au serikali za Kiislamu ni haramu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Mtukufu Ayatullah Makarem Shirazi amesisitiza kuwa: Kila mtu au utawala wowote unaomtishia kiongozi wa Mapinduzi na marjaiya au—Mungu apishe mbali—unaofanya jaribio la kuwadhuru, kwa lengo la kuupiga pigo Umma wa Kiislamu na utawala wake, una hukumu ya "muharib", na aina yoyote ya ushirikiano au kuutia nguvu kutoka kwa Waislamu au serikali za Kiislamu ni haramu.

Hapa chini soma uchambuzi wa matukio ya hivi karibuni kwa mtazamo wa Mtukufu Ayatullah Makarem Shirazi:

Matukio ya hivi karibuni

Matukio na visa vya siku za hivi karibuni vimeumiza mioyo ya kila mwanadamu mwenye huruma. Taifa hili limetoa gharama kubwa kwa ajili ya uhuru na heshima yake, na sasa ambapo adui, kwa umakini zaidi kuliko hapo awali, kwa dhana yake mwenyewe anapanga njama za kulipiga pigo taifa hili na watu wake, ni lazima tulinde umoja wetu zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Kwa sababu hiyo, naona ni muhimu kuwaelekeza wapendwa wenu kwenye mambo machache ya msingi na ya lazima. [1]

Maisha ya watu yanahitaji hatua za vitendo

Kuwepo kwa matatizo katika hali ya soko na maisha ya watu kunawaumiza wote. Katika hali hii, serikali ilitenga kiasi fulani cha fedha kusaidia maisha ya wananchi, jambo ambalo lilikuwa jema; lakini mara moja ikakata ruzuku ya fedha za kigeni kwa bidhaa za msingi, jambo lililosababisha athari katika bidhaa zote na kuongeza shinikizo kwa wananchi. [2]

Hakuna shaka kuwa hali ngumu ya maisha, kupanda kwa bei kusikodhibitika na kutokuwa na uthabiti wa bei ni miongoni mwa sababu kuu za kutoridhika kijamii. Wafanyakazi na wale wanaopokea mishahara ya kudumu hawawezi kuendana na ongezeko la kila siku la bei, na jambo hili husababisha maandamano. Lakini wote, hasa wasomi na wenye ushawishi katika kila ngazi ya jamii, wanapaswa kuwa makini ili madai haya ya haki yasigeuke kuwa fursa ya kutumiwa vibaya. [3]

Bila barakoa

Katika machafuko na matukio ya kigaidi yaliyotokea hivi karibuni nchini, barakoa imeanguka usoni mwa waharibifu, na hata Israel imekiri kuwa na nafasi katika machafuko haya.

Bila shaka, kitendo chochote cha kuharibu misikiti, maeneo ya umma, makazi ya wafanyabiashara, benki na mali nyingine za watu ni aina ya kupigana na mfumo wa Kiislamu na Uislamu wenyewe. [4]

Udanganyifu mkubwa

Rais wa Marekani amejaa udanganyifu, na mtaji wake mkuu Trump ni uongo. Trump ana dhana ya kuporomoka kwa mfumo wa Kiislamu. Viongozi wa Marekani walidhani kuwa kwa shinikizo la kiuchumi, watu wa Iran wangeinama mbele yao na kuja kwenye meza ya mazungumzo, lakini wananchi walionyesha wazi kuwa hilo ni wazo la uongo tu.

Bila shaka, kufanya mazungumzo na Marekani isiyoheshimu ahadi yoyote si jambo la mantiki wala la busara; haifai kufanya mazungumzo tena na nchi ambayo haizingatii ahadi, na hata hukiuka hadharani mikataba iliyosainiwa mbele ya kamera.

Vikwazo pia ni silaha inayotokana na udhaifu na kushindwa; nchi huweka vikwazo pale ambapo haina hatua nyingine yoyote zaidi ya vikwazo, na kwa neema ya Mwenyezi Mungu, njama hii ya maadui pia itashindwa kwa kusimama imara na kustahimili kwa wananchi na viongozi. [5]

Tunaujali sana uongozi wa Umma

Viongozi waliokata tamaa wa Marekani, wakiwa katika hali ya udhaifu mkubwa na kwa upumbavu, wamefungua midomo yao na kuanza kumtishia Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Kuwepo kwa kiongozi kama mlinzi wa misingi ya Kishia, bali ya Umma mzima wa Kiislamu, ni sehemu nyeti katika itikadi yetu, na hakuna Muislamu mwema na huru atakayevumilia vitisho hivi. Kwa hiyo, ni lazima Waislamu na watu huru duniani kote, kwa njia yoyote iwezekanavyo, wasisitize kumuunga mkono na kulaani aina yoyote ya dharau, ili wote wajue kuwa mataifa duniani yamesimama dhidi yao.

Vikosi vya ulinzi pia, kama ambavyo hadi sasa kwa nguvu vimefanya uwanja uwe mgumu kwa adui, vinapaswa kwa ubunifu, na mashambulizi dhidi ya upande wa pili, kumfanya adui asithubutu hata kuwaza mawazo au vitisho vya aina hii. [6]

Kuanguka ni kwa hakika

Marekani ndiyo nchi kuu inayowadhulumu watu wake na watu wengine duniani kwa ujumla. Tunaamini kwamba utawala wa aina hii hautadumu, kwa sababu dhulma haidumu milele. Kwa hiyo, mapema au baadaye wataondolewa, na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, mustakabali utakuwa mikononi mwa wanaotafuta haki.

Kama Qur’ani Tukufu inavyosema wazi: “Na ardhi watairithi waja Wangu wema.” [7]

InshaAllah, kwa kudhihiri kwa Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake), dunia yote itaingia chini ya bendera ya uadilifu wa Mwenyezi Mungu. [8]

Hukumu ya muharib

Kila mtu au utawala wowote unaomtishia kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu na marjaiya, au—Mungu aepushe mbali—unaofanya jaribio la kuwadhuru, kwa lengo la kuupiga pigo Umma wa Kiislamu na mamlaka yake, una hukumu ya muharib, na aina yoyote ya ushirikiano au kuutia nguvu kutoka kwa Waislamu au serikali za Kiislamu ni haramu. Ni wajibu kwa Waislamu wote duniani kuwafanya maadui hawa wajutie maneno na makosa yao, na iwapo watapata tabu au hasara, watapata thawabu ya mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu, InshaAllah. [9]

Chuki za Trump dhidi ya Sepah

Rais wa Marekani, kwa lengo la kuleta migawanyiko na kulipiza kisasi, aliliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah), ambalo ni miongoni mwa vinara wa mapambano dhidi ya ugaidi, katika orodha ya makundi ya makundi ya kigaidi, akidhani kuwa kwa tuhuma hii ataweza kuleta mpasuko katika safu za taifa letu na kulitenga jeshi hilo na wananchi.

Lakini kinyume na matakwa na malengo ya viongozi wa Marekani, nafasi na hadhi ya Sepah miongoni mwa wananchi ilizidi kuwa ya juu na imara zaidi.

Watu wote wenye akili duniani wanaamini kuwa lau Sepah isingetoa msaada, magaidi wakatili wa Daesh—waliozaliwa na sera za kigaidi za Wamarekani—wangekuwa wameiteka Baghdad, Damascus na hata Beirut. Bila shaka, kuiweka Sepah kwenye orodha ya magaidi na serikali ambayo yenyewe ni kinara wa ugaidi duniani ni kitendo cha kipumbavu. Adui alikusudia kuleta migawanyiko na kulisambaratisha taifa letu, lakini kwa sifa njema ya Mwenyezi Mungu, alipata matokeo ya kinyume. [10]

Njama ya kuivamia Iran

Marekani inalenga kupanua ushawishi wake wa kikanda; ili kufikia lengo hili, inalazimika kuwasha moto wa vita katika kila kona ya dunia. Hakuna hata mmoja wa wachochezi wa vita katika dunia ya kimaada ya leo anayesema kuwa anapigana kwa ajili ya radhi ya Mwenyezi Mungu; bali hutumia visingizio ili kuanzisha vita na kufikia malengo yake, na chini ya kivuli cha visingizio hivi huanzisha vita.

Haki za binadamu!

Katika baadhi ya nchi walizozilenga kivita "haki za binadamu" hutumika kama kisingizio, na kwa propaganda kubwa huandaa fikra za watu duniani kwa ajili ya vita dhidi ya nchi hiyo; kisha chini ya kivuli cha kauli hii ya uongo, huishambulia na kuikalia, huku kiuhakika wakifikiria malengo yao binafsi.

Demokrasia!

Kisingizio kingine cha wachochezi wa vita ni “Demokrasia”. Waliivamia Iraq kwa madai ya kuuangusha utawala wa kidikteta wa Saddam na kuleta demokrasia; lakini huu ulikuwa ni mwonekano wa nje tu, kwani lengo lao la kweli lilikuwa visima vya mafuta vya Iraq.

Uhuru!

Kisingizio kingine cha uongo ni ukosefu wa uhuru katika nchi husika. Kwa jina la kutafuta uhuru, huikalia nchi nyingine, na kwa jina la uhuru huwafanya watu na serikali zake kuwa mateka wa matamanio yao.

Haya ndiyo malengo yao ya kuleta vita katika dunia ya leo, yanayotajwa mara kwa mara katika pembe mbalimbali za dunia chini ya vifuniko vya haki za binadamu, demokrasia na uhuru. [11]

Neno la mwisho: (Iran Imara; kutoka azma hadi utekelezaji)

Watoto wangu wapendwa! Msiwaruhusu mawakala wa adui kunufaika na madai yenu ya haki na kwa kisingizio chake wakayatusi matakatifu, wakaharibu mali na maeneo ya umma na misikiti, na hata kuvamia mali binafsi na heshima ya watu; ni lazima mjitenganishe nao waziwazi.

Wapendwa wangu! Sote tunapaswa kusaidiana ili walinzi wa usalama warejeshe utulivu kamili katika jamii. Angalieni Syria, Libya na mfano wake, jinsi walivyopoteza heshima na usalama wao, na adui wa nje akawatawala. Adui huyu wa nje hatupendi, bali anatafuta kulipiga pigo taifa hili na kutwaa rasilimali zake.

Watu wote wa Iran na makabila yote—Waturuki, Wakurdi, Waluri, Waarabu, Wafarsi, Wabaluchi na wengine—wanapaswa kujua kuwa ni Iran moja iliyo imara na iliyoungana pekee inayoweza kuhakikisha usalama na ustawi wa wote.

Ni jukumu la taasisi za kitamaduni zenye ushawishi, na hasa familia, kuwaelekeza vijana na watoto kwa kufafanua ukweli, kueleza nguvu na mambo yanayotoa matumaini; kwani mtaji wa nchi hii ni nyoyo hizi safi ambazo sasa zimo katika hatari ya mashambulizi ya wasiwasi na ufisadi. [12]

Kwa hakika, kilichotupa na kitaendelea kutupa nguvu katika nyanja zote ni imani ya watu wetu na wapiganaji wetu. Kwa hiyo, ni lazima watu wote na Waumini, katika hali hizi ngumu, kwa ikhlasi wanyanyue mikono yao kwa Mwenyezi Mungu, na binafsi na kwa pamoja wasipuuzie dua, unyenyekevu na tawasuli kwa Maimamu watoharifu (amani iwe juu yao); kwani adui wenu awe nani, bado:
“Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao.” [13]

Natumai katika siku na nyakati hizi tukufu (za Mwezi wa Sha‘ban), nchi hii na mfumo wake, kwa uangalizi wa Imam wa Zama, Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake, kwa ushirikiano wa wananchi na viongozi, itahifadhiwa dhidi ya kila shari ya wenye nia mbaya, InshaAllah. [14]

Vyanzo:

Hotuba na matamshi ya Mtukufu huyo:

[1] Maandishi ya ujumbe wa Mtukufu Ayatullah al-‘Udhmaa Makarem Shirazi kufuatia matukio ya hivi karibuni nchini, tarehe 20/10/1404.

[2] Hotuba za Mtukufu Ayatullah al-‘Udhmaa Makarem Shirazi katika mkutano na wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom, tarehe 22/10/1404.

[3] Hotuba za Mtukufu Ayatullah al-‘Udhmaa Makarem Shirazi katika mkutano na Mkuu wa Shirika la Habari la Taifa, tarehe 12/10/1404.

[4] Hotuba za Mtukufu Ayatullah al-‘Udhmaa Makarem Shirazi katika mkutano na wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom, tarehe 22/10/1404.

[5] Hotuba za Mtukufu Ayatullah al-‘Udhmaa Makarem Shirazi katika mkutano na Waziri wa Elimu, Utafiti na Teknolojia, tarehe 28/3/1398.

[6] Maandishi ya ujumbe wa Mtukufu Ayatullah al-‘Udhmaa Makarem Shirazi kufuatia kitendo cha dharau dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, tarehe 29/3/1404.

[7] Surat Al-Anbiyaa, Aya ya 105.

[8] Hotuba za Mtukufu Ayatullah al-‘Udhmaa Makarem Shirazi katika mkutano na Louis Farrakhan, kiongozi wa Harakati ya Umma wa Kiislamu nchini Marekani, tarehe 15/7/1397.

[9] Maandishi ya jibu la Mtukufu Ayatullah al-‘Udhmaa Makarem Shirazi kwa swali la kisheria (istiftaa) kuhusu vitisho vya Marekani dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, tarehe 8/4/1404.

[10] "Mpango Mpya katika Masuala ya Maadili", Juzuu ya 2, ukurasa wa 244.

[11] "Wanakuuliza", ukurasa wa 68.

[12] Maandishi ya ujumbe wa Mtukufu Ayatullah al-‘Udhmaa Makarem Shirazi kufuatia matukio ya hivi karibuni nchini, tarehe 20/10/1404.

[13] Surat Al-Fat’h, Aya ya 10; (maandishi ya ujumbe wa Mtukufu Ayatullah al-‘Udhmaa Makarem Shirazi, kufuatia kitendo cha dharau dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, tarehe 29/3/1404).

[14] Maandishi ya ujumbe wa Mtukufu Ayatullah al-‘Udhmaa Makarem Shirazi kufuatia matukio ya hivi karibuni nchini, tarehe 20/10/1404.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha