Alhamisi 22 Januari 2026 - 22:59
Aina yoyote ya kumshambulia au kumdhuru Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ina hukumu ya “muharib” / Sielewi watu mashuhuri wanaonyamazia wanafikiria nini

Hawza/ Mtukufu Ayatullah Nouri Hamedani alisisitiza: Rais wa Marekani ajue kwamba yeyote atakayethubutu kumshambulia au kumdhuru Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ni “muharib” (mtu anae upiga vita uislamu). Hili tumekwishalieleza hapo awali pamoja na hoja zake za kifiqhi. Sisi tunaona kumuunga mkono kiongozi ni wajibu wa kisheria katika dini.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Mtukufu Ayatullah Nouri Hamedani katika mkutano na kundi la maimamu wa misikiti wa mkoa wa Tehran, alieleza kuwa jukumu la wanazuoni ni muhimu sana na lina athari kubwa, alisema: Tuko katika kipindi maalumu, na leo adui ameelekeza mashambulizi yake yote kupitia mitandao ya kijamii dhidi ya wanazuoni wa dini; kwa hiyo, wanazuoni nao wanapaswa kuwapo uwanjani. Leo si jukumu la imamu wa msikiti kuvaa joho, kwenda kuswali tu na kutojali hali za watu; wanazuoni hawapaswi kuacha uwanja wazi.

Huku akikosoa vikali ukimya wa watu mashuhuri katika fitna au kutoa misimamo kwa kuchelewa, alibainisha: Sielewi hawa mabwana wanafikiria nini? Je, wanafikiri Jamhuri ya Kiislamu ikiporomoka, adui ataacha athari yoyote ya Mwenyezi Mungu, Qur’ani na Ahlul-Bayt (amani iwe juu yao) ibaki? Sote tuliona katika fitna ya hivi karibuni ni nini kiliwapata watu, misikiti na kwwnye husseiniyya. Tuliona jinsi walivyoichoma Qur’ani.

Akaendelea kusema: Je, kweli yote haya yalikuwa kwa sababu ya masuala ya kiuchumi? Bila shaka watu wanakabiliwa na hali ngumu za maisha, lakini wahalifu walioua watu na kuchoma kila mahali hawakuwa watu wa kawaida.

Marji' huyu wa taqlid aliongeza kusema: Rais wa Marekani anakuja hadharani na kuwapa matumaini wachochezi wa vurugu, na hivi karibuni pia anamtishia Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi. Ingawa hastahili kujibiwa, lakini anapaswa kujua kwamba Ayatullah Khamenei, kama faqihi na kiongozi wa umma, yeyote atakayethubutu kumshambulia ni “muharib”. Tumekwishaeleza hili hapo awali na kutoa hoja zake za kifiqhi. Tunatarajia wanazuoni wote washuke uwanjani na kumuunga mkono kiongozi. Sisi hatuoni kumuunga mkono kiongozi kuwa ni suala la kisiasa pekee, bali ni wajibu wa kisheria wa dini.

Mtukufu Ayatullah Nouri Hamedani aliendelea kusema: Mimi hushangaa sana ninapoona katika fitna baadhi ya watu wananyamaza au wanatoa maoni kwa kuchelewa, wakisubiri kuona mambo yataelekea wapi ndipo wachukue msimamo, ilhali katika wakati ambao ni wazi kabisa haki iko wapi na batili iko wapi.

Marji' huyu wa taqlid alisisitiza: Hatuna shaka kwamba nchini lazima kuwe na mshikamano na kuepuka migawanyiko, na wote wanapaswa kuwa na umoja. Lakini hili halimaanishi kwamba baadhi ya watu wafanye lolote watakalo na wengine wote wakae kimya, au chombo cha usimamizi kisifanye kazi yake kwa kisingizio cha kusema tunataka mshikamano.

Mwisho, Mtukufu Ayatullah Nouri Hamedani alisisitiza kwa kusema: Mshikamano maana yake ni kusaidiana katika kutatua matatizo ya watu. Kiongozi amesema: “Maafisa wanapaswa kufanya kazi mara mbili”, yaani waongeze juhudi katika kutekeleza majukumu yao. Hii ina maana kwamba mhimili wa mahakama uzidishe juhudi katika kushughulikia kesi, Bunge lizidishe usimamizi wake, na serikali ijitahidi mchana na usiku kutatua matatizo ya wananchi bila kuchoka.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha