Jumapili 28 Desemba 2025 - 16:10
Dunia ya leo inahitajia Mfumo wa haki wa Kiislamu, kitaifa na kimataifa

Hawza/ Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ujumbe wake kwenye mkutano wa mwaka wa Umoja wa Jumuiya za Kiislamu zaa Wanafunzi barani Ulaya amesema: Dunia ya leo inahitajia kuwepo mfumo wa haki wa Kiislamu, kitaifa na kimataifa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Khamenei katika ujumbe wake kwenye mkutano wa hamsini na tisa wa mwaka wa Umoja wa Vyama vya Kiislamu vya Wanafunzi barani Ulaya, huku akirejea kushindwa kwa uvamizi mzito wa jeshi la Marekani pamoja na zao lake la aibu katika eneo hili, kutokana na ubunifu, ujasiri na kujitolea kwa vijana wa Iran, alisisitiza kwamba: chanzo kikuu cha vurugu na mfadhaiko wa madhalimu mafisadi na waharibifu si mjadala wa nyuklia, bali ni kuinuliwa bendera ya kupambana na mfumo dhalimu na udikteta wa mfumo wa ubeberu duniani, pamoja na kuelekea kwenye mfumo wa haki wa kitaifa na kimataifa wa Kiislamu kutoka upande wa Iran.

Matini ya ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu

Vijana wapendwa!
Mwaka huu, nchi yenu, kwa baraka ya imani, umoja na kujiamini, imepata hadhi na uzito mpya duniani. Uvamizi mzito wa jeshi la Marekani na zao lake la aibu katika eneo hili, umeshindwa na ubunifu, ujasiri na kujitolea vijana wa Iran. Imethibitika kwamba taifa la Iran, kwa kutumia uwezo wake tu, chini ya kivuli cha imani na matendo mema, na katika kukabiliana na madhalimu mafisadi na waonevu, linaweza kusimama imara na kufikisha wito wa maadili ya Kiislamu duniani kwa sauti kubwa zaidi kuliko wakati wowote ule.

Huzuni kubwa kutokana na kuuawa kishahidi idadi ya wanazuoni, makamanda na kundi la watu wetu wapendwa, haikuweza na wala haitaweza kuwazuia vijana wa Iran wenye azma thabiti. Familia za mashahidi hao, zenyewe zimo miongoni mwa viongozi wa mbele katika harakati hii.

Suala si mzozo wa nyuklia wala mambo yanayofanana na hilo. Tatizo ni kupambana na mfumo dhalimu na uonevu wa mfumo wa ubeberu katika dunia ya leo, na kuelekea kwenye mfumo wa haki wa kitaifa na kimataifa wa Kiislamu. Hili ndilo dai kubwa ambalo Iran ya imebeba bendera yake, na ambalo limewachanganya na kuwakasirisha madhalimu mafisadi na waharibifu.

Ninyi wanafunzi, hususan mlioko nje ya nchi, mna sehemu ya jukumu hili kubwa juu ya mabega yenu. Zikabidhini nyoyo zenu kwa Mwenyezi Mungu, tambueni uwezo wenu, na elekezeni jumuiya zenu kwenye mwelekeo huu.

Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, na ushindi kamili unawasubiri, InshaAllah.

Sayyid Ali Khamenei

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha