Jumanne 9 Desemba 2025 - 16:45
Lebanon Kamwe Haitatolewa Zawadi Bure Kutokana na Tamaa za Wazayuni na Marekani

Hawza/ Chama cha Hizbullah kiliandaa hafla katika Husseinia ya mji wa Hlabta, kutokana na mnasaba wa kumbukizi ya mwaka wa shahada ya Sheikh Adnan Ali Saifuddin.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hizbullah iliandaa hafla katika Husseinia ya mji wa Hlabta, kutokana na mnasaba wa kumbukizi ya mwaka wa shahada na kutoweka Sheikh Adnan Ali Saifuddin. Katika hafla hiyo, Dkt. Iyhab Hamadeh, mbunge wa Bunge la Lebanon na mjumbe wa kikundi cha uaminifu kwa upande wa Muqawama, alihudhuria pamoja na idadi ya viongozi wa kisiasa, wajumbe wa mabaraza ya miji na vijiji, pamoja na wanaharakati wa kijamii.

Iyhab Hamadeh katika hotuba yake alisisitiza kuwa Lebanon, pamoja na mipaka yake yote, rasilimali zake na vipengele vyake vyote vya wananchi, itabaki kama ilivyo, na kamwe haitawasilishwa kama zawadi ya bure mbele ya tamaa za Kizayuni na Kimarekani.

Aliendelea kusema: mwelekeo wa kisiasa tunaoukubali, kama ulivyotajwa katika hotuba za Rais wa Jamhuri na katika tamko la mawaziri la serikali, ni lazima uwe katika kuhudumia uhuru wa ardhi, kuwaachilia huru wafungwa, pamoja na ujenzi na uendelezaji wa nchi; siyo kuishia katika kuulinda utawala wa kikoloni au kumtumikia adui.

Katika hafla hiyo, wasia wa shahidi ulioneshwa, mwana wa shahidi alitoa hotuba yenye kugusa hisia, na mwishoni hafla ilihitimishwa kwa majlisi ya maombolezo ya Imam Husseini (as).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha