Jumatano 3 Desemba 2025 - 18:14
Serikali ya Ufaransa Yalegeza Kamba Kuhusiana na Marufuku ya Hijabu kwa Wasichana Walio Chini ya Umri wa Miaka 18

Hawza/ Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na kampeni kubwa kwenye vyombo vya habari kuhusu pendekezo la kupiga marufuku hijabu hata kwa watoto, jambo ambalo limechochea maudhi na wasiwasi mkubwa katika maoni ya umma nchini Ufaransa. Mpango wa kupiga marufuku hijabu kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 18 uliwasilishwa bungeni na Laurent Wauquiez, ambaye anajulikana kwa chuki dhidi ya Uislamu, lakini umeakataliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya Tarjama ya SShirika la Habari la Hawza, Bw. Nonbez, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa kwa wakati huo, alisema: “Sikubaliani na pendekezo hili kwa sababu litasababisha maudhi na hofu kwa familia za raia Waislamu wa Kifaransa pamoja na wasichana wao walio baleghe, na huenda likawaathiri kisaikolojia.”

Awali, alikuwa Mkuu wa Polisi wa Paris na hivi karibuni aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani. Hata hivyo, kutokana na kuongezeka kwa ushawishi wa kisiasa na kijamii wa mrengo wa kulia wenye msimamo mkali na chuki dhidi ya dini nchini Ufaransa, kwa masikitiko makubwa mijadala ya kueneza kutokuwa na dini pamoja na sheria zinazounga mkono hali hiyo imezidi kushika kasi, jambo ambalo limesababisha mivutano mingi ya kisiasa nchini humo.

Mwanzoni mwa mwaka huu pia, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, alipendekeza kupiga marufuku hijabu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 15 katika maeneo ya umma, lakini pendekezo hilo halikuidhinishwa rasmi.

Kwa mujibu wa sheria za sasa za Ufaransa, watumishi wa umma, walimu na wanafunzi wa shule za serikali hawaruhusiwi kuvaa alama za dini zinazoonekana wazi, zikiwemo msalaba wa Kikristo, kipa ya Kiyahudi, kilemba cha Wasikh na hijabu ya Kiiislamu ndani ya majengo ya serikali na shule za umma, na aina yoyote ya udhihirisho wa dini inaoyo onekana hadharani hutambuliwa kuwa kosa la kisheria.

Chanzo: MOROCCO WORLD NEWS

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha