Jumatano 3 Desemba 2025 - 12:14
Kumswalia Mtume na Athari Zake Katika Kutimizwa Haja kwa Mtazamo wa Ayatullah Udhma Jawadi Amoli

Hawza/ Mtukufu Ayatullah Jawadi Amoli amesema: kumswalia Mtume na thawabu zake ni miongoni mwa kheri na malipo bora na ya juu kabisa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Hawza, Mtukufu Ayatullah Jawadi Amoli katika maelezo yake kuhusiana na mada ya “dhikri yenye baraka ya kumswalia Mtume,” alisema: Kumswalia Mtume na thawabu zake ni miongoni mwa kheri na malipo bora kabisa. Imam Swa'diq (a.s) amesema: Jina la Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) linapotamkwa kwa ulimi, basi zidisheni kumswalia, kwani atakayemswalia Mtume (s.a.w.w) mara moja, safu elfu moja za Malaika humswalia mara elfu moja, na kila alichokiumba Mwenyezi Mungu pia humswalia na humtolea salamu. Na yule asiye na hamu wala shauku ya kumswalia Mtume (s.a.w.w), huyo ni mjinga na mwenye kujigamba; na Mwenyezi Mungu, Mtume Wake pamoja na Ahlul-Bayt (a.s) hujitenga naye.

Adabu ya dua na maombi ni kuanza kwa kumtaja, na kumsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha baada ya kutuma salamu juu ya Ahlul-Bayt wa Ismah na Tohara (a.s), ndipo haja iwasilishwe. Bila ya salamu hizi, dua haipokelewi. Na ikiwa mtu atapata jambo fulani bila ya kuwaswalia Ahlul-Bayt (a.s), basi huo ni mtihani, si rehema wala kuitikiwa kwa dua. Kama alivyosema Imam Swa'diq (a.s):
“Dua huendelea kuwa imezuiliwa hadi utakapomswailia Muhammad na Aali zake.”
Kwa sababu hiyo, Amirul-Muuminin (a.s) alisema: Mnapomwomba Mwenyezi Mungu kutimizwa kwa haja fulani, anzeni kwa kumswalia Mtume mtukufu (s.a.w.w). Na Imam Sajja'd (a.s) pia huwafundisha waombaji adabu hii katika dua za Sahifa Sajjadiyya.

Siri ya jambo hili, kama alivyokuwa akieleza mwalimu, Allama Tabataba’i (Mwenyezi Mungu amrehemu), katika darsa zake, ni kwamba: Mtu anapowaswalia Ahlul-Bayt wa Ismah na Tohara (a.s), huwa anamwomba Mwenyezi Mungu awateremshie rehema familia hii; na dua hii hukubaliwa. Rehema ya Mwenyezi Mungu inapowafikia wao, huwafikia pia Mashia wao wote, ambaye mwombaji ni miongoni mwao. Na kwa namna hii, chini ya kivuli cha rehema ya Mwenyezi Mungu na kwa baraka za zile nyuso tukufu za nuru, haja ya mwombaji hutimizwa.

Elimu na njia ya uchamungu uk: 415 - 146

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha