Alhamisi 23 Oktoba 2025 - 12:59
Mataifa Huru Duniani yamegundua uwongo na hila za Marekani na Israeli

Hawza/ Hujjatul-Islam Maqsood Ali Domki katika hotuba yake alisema: damu safi ya mashahidi wa muqawama imefunua uso wa udanganyifu wa Marekani na Israeli na kuonesha ukweli wa dhulma inayoyakabili mataifa yaliyobanwa mbele ya dhamiri ya ulimwengu.

Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya  Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Maqsood Ali Domki, mshiriki mtendaji katika Baraza la Muungano wa Waislamu wa Pakistan, katika mkutano wa kila mwaka wa Shirika la Wanafunzi wa Imamia Pakistan uliofanyika katika mji wa Nawabshah, jimbo la Sindh, akitaja mabadiliko ya hivi karibuni katika eneo na kuendelea kwa muqawama wa watu wa Palestina, alisema: “Leo mataifa huru duniani yamekubali wazi dhulma zinazo elekezwa kwenye mhimili wa muqawama, na uso halisi wa Marekani na utawala wa Kizayuni, pamoja na udanganyifu, hila na ukandamizaji wao, umefichuka kwa wote.”

Aliongeza kubainisha nafasi ya damu ya mashahidi katika kuuamsha umma: “Damu safi ya mashahidi wa muqawama imelifanya suala la Palestina kuwa wazo kuu na tatizo la kimataifa. Mashahidi waliodhulumiwa kutoka Lebanon, Yemen, Iran, Ghaza na Palestina kwa kujitoa kwao wamebainisha wazi uhalali na uaminifu wa njia ya muqawama, na wamefichua uso wa kinafki, udanganyifu na uhalifu wa utawala wa Kizayuni na wafuasi wake wa Magharibi kwa mataifa yote.”

Mwanazuoni huyo wa Pakistani, akielezea hali ya uwanja wa mapigano huko Ghaza, alisisitiza kuwa: “Utawala wa Kizayuni kwa vitendo umeshindwa kwenye vita hiiv, wakati mashujaa wa Palestina na wapiganaji wa mhimili wa muqawama wamesimama na ushindi. Hatimaye, Israeli italazimika kujiondoa kutoka katika ardhi zilizokaliwa za Palestina na kuacha ukoloni wake; kwa sababu haki daima itaishi na uongo utakufa.”

Akilaumu baadhi ya harakati wanaotafuta fursa ndani ya Uislamu, alisema: “Wale walioungana pamoja Marekani na Israeli wameifanyia khiyana Palestina na mashahidi wa Ghaza na ni wadanganyifu kwa umma wa Kiislamu, na wakati wa malipo yao umekwisha wadia.”

Kwa kumalizia na kuutaka umma wa Kiislamu kuwa pamoja, alisema: “Sasa ni wakati wa umoja wa Uummah wa Kiislamu, tukitegemea basira za Qur’ani, umoja na azimio thabiti la muqawama, ili kwa ajili ya ukombozi wa mji wa Qibla ya kwanza ya Waislamu, Beitul Muqaddas, tuungane na kusimama pamoja na kwa moyo mmoja na kwa uvumilivu, na kwa mshikamano tushughulikie na kuondoa dhulma pamoja na ukoloni kutoka katika ardhi za Kiislamu.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha