Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini ya ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni kama ifuatavyo:
Bismillahir Rahmânir Rahîm
Nawapongeza vijana mashujaa wa mieleka ya farangi.
Azma thabiti na juhudi ngumu zenu pamoja na ndugu zenu wa mieleka ya Azad, zimei furahisha jamii na kuipa nchi heshima, namuomba Mwenyezi Mungu awajalie utukufu na ushindi, na ninatoa pongezi kwa mwanamichezo, kocha na meneja.
Sayyid Ali Khamenei
30 Shahrivar 1404 Hsh
Timu ya Taifa ya Mieleka ya Farangi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, baada ya miaka 11 na kwa mara ya pili, imeweza kusimama kwa uimara katika jukwaa la ubingwa wa dunia katika mashindano ya Zagreb 2025.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya michezo ya Iran ambapo Timu ya Taifa ya Mieleka ya Azad na ya Farangi zimefanikiwa kwa pamoja kutwaa ubingwa wa dunia katika mashindano ya kipindi kimoja.
Maoni yako