Jumatano 17 Septemba 2025 - 00:23
Nahjul-Balagha ni Kitabu chenye Mageuzi na Mapinduzi / Wanafunzi wakike wa Hawza wana nafasi ya Kihistoria katika kuiongoza Dunia Mpya

Hawza/ Mkurugenzi wa Hawza Nchini Iran ameitaja Nahjul-Balagha kuwa ni kitabu cha mageuzi na mapinduzi, na kusisitiza: Hawza za wanawake zinapaswa kuanzisha sura maalum ya kuongeza maarifa kuhusu Mtume (s.a.w.w), hasa kwa mtazamo wa Nahjul-Balagha; kwani kuitilia mkazo Nahjul-Balagha ni jambo lililoelezwa wazi na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza A‘rafi, katika hafla ya pamoja ya kuanza mwaka mpya wa masomo hawza ya Jami‘atuz-Zahra (s.a), iliyofanyika leo tarehe 25 Shahrivar 1404 (kwa kalenda ya Irani) katika ukumbi wa Bidari ya Kiislamu huko Qum, huku akikumbushia kumbukumbu ya kuwasili kwa Bibi Fatima Ma‘suma (s.a) mjini Qum, alisema:

Nuru ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w) katika nyanja zote ulimwenguni ndio nuru ya mwanzo na mwenge wa kwanza wa uongofu. Dunia iling‘ara kwa taa ya Mtume (s.a.w.w), Uislamu uliingia katika ustaarabu na dunia mpya kwa uwepo wake, na hatima ya ulimwengu pia itakamilishwa kwa nuru yake angavu.

Uakisi wa Mtume (s.a.w.w) katika Nahjul-Balagha

Rais wa Baraza la Sera za Hawza za Wanawake aliongeza: Taswira ya Mtume (s.a.w.w) katika kioo cha Nahjul-Balagha ni miongoni mwa taswira za kuvutia zaidi, kauli za kuvutia na fasaha za Amirul-Mu’minin (a.s) katika zaidi ya sehemu 40 za Nahjul-Balagha kuhusu Mtume (s.a.w.w) zinaunda mfumo wa kielimu na mkusanyiko wa kuvutia katika kumjua Mtume na kuuelewa utu wake.

Akasema tena: Hawza za wanawake zinapaswa kuanzisha sura maalum ya kuongeza uelewa kuhusiana na Mtume (s.a.w.w), kwa mtazamo wa Nahjul-Balagha, jambo ambalo limepewa msisitizo wa pekee na Kiongozi wa Mapinduzi.

Mtume katika maneno ya Imam Ali (a.s)

Ayatullah A‘rafi alifafanua: Imam Ali (a.s) katika Nahjul-Balagha amezungumzia mambo mbalimbali kuhusu Mtume (s.a.w.w); ikiwa ni pamoja na: historia ya kijamii ya Warabu na mazingira ya wakati wa utume, nafasi ya familia ya Mtume (s.a.w.w), pamoja na sifa zake binafsi.

Kisha alisoma sehemu ya dua ya Imam Ali (a.s):

«وَ داعِمَ الْمَسْمُوكاتِ، وَ جابِلَ الْقُلُوبِ عَلى فِطْرَتِها، شَقِيِّها وَ سَعیدِها؛ اِجْعَلْ شَرائِفَ صَلَواتِكَ، وَ نَوامِیَ بَرَكاتِكَ عَلى مُحَمَّدٍ عَبْدِكَ وَ رَسُولِكَ»

“Ee Mwenye kushikilia mbingu zilizoinuliwa, na Muumbaji wa nyoyo juu ya asili yake, za mwenye furaha na mwenye taabu; weka rehma bora na baraka tele zaidi juu ya Muhammad, mja wako na Mtume wako.”

Akaongeza kuwa: Katika khutba hii, Imam Ali (a.s) anasisitiza juu ya ubudiya (uabdifu) na risala (utume) wa Mtume (s.a.w.w), kisha anasema:


 «الْخاتِمِ لِما سَبَقَ»

yaani Mtume aliyehitimisha mlolongo wa mitume.

Ayatullah A‘rafi akasema: Uhitimisho huu ni wa kihistoria kwa wakati, lakini kwa hadhi na cheo, Mtume (s.a.w.w) yupo mwanzo. Kwa sababu mwanadamu ilibidi kwanza aandaliwe ili aweze kupokea Qur’an na ujumbe wa Mtume wa Mwisho, hazina kubwa ya maarifa ya tauhidi na elimu ya Kiungu ambayo ipo katika Qur’an na sunna ya Mtume na Ahlulbayt (a.s) haingeweza kutolewa mwanzoni mwa uumbaji, kwani wanadamu hawakuwa na uwezo wa kuibeba.

Qur’an na upekee wa Mtume (s.a.w.w)

Akaendelea kusema: Upeo wa tauhidi uliomo ndani ya Qur’an haukuwahi kuwepo katika falsafa ya Wagiriki au ya kale, hata kilichokuwepo hakikuwa cha kutegemewa au hakina yakini, lakini Qur’an imefunua tauhidi kwa namna ambayo haijulikani katika fikra za kifalsafa au kiirfani.

Ayatullah A‘rafi akaongeza: Imam Ali (a.s) pia anasema: 


«وَ الْفاتِحِ لِمَا انْغَلَقَ»

Yaani “Mfunguaji wa yale yaliyokuwa yamefungika.”

Hii ni dalili kwamba kupitia Mtume na Qur’an, milango mipya ilifunguliwa katika imani, itikadi, fikra za kijamii, mifumo ya kifikra, masuala ya kifalsafa, fiqhi na maadili, mambo ambayo kabla yake yalikuwa yamefungika.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha