Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza Sayyid Zawar Husayn Naqvi, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Ja‘fariyya Kashmir Pakistan, katika ujumbe wake alibainisha kuwa shambulio la Israel dhidi ya viongozi wa ngazi ya juu wa Hamas mjini Doha ni tendo la jinai na hatari kubwa, ambalo halikulenga mamlaka ya Qatar pekee, bali limeuweka mashakani usalama na heshima ya Umma mzima wa Kiislamu.
Akaongeza kusema: Shambulio hili lisingewezekana bila uratibu wa Marekani na nguvu za Magharibi, na kwa mara nyingine imedhihirika kuwa uzayuni hauna nia njema yoyote kwa nchi za Kiislamu, Ardhi, uongozi, pamoja na vituo vya kielimu na kiteknolojia vya nchi za Kiislamu daima vimekuwa shabaha ya njama za Kizayuni.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Ja‘fariyya Kashmir alikosoa kimya kinachofanywa na taasisi za kimataifa kutokana na jinai hiz na kusema: Kimya hiki kimewafanya Wazayuni kuwa na jeuri zaidi na kimewachochea kuvunja sheria na kufanya vitendo vya uvamizi, hivi sasa Umma wa Kiislamu unapaswa kuamka, kuungana na kwa kutumia nguvu zake kutoa majibu madhubuti kwa Israel.
Alisisitiza kuwa: Shambulio hili ni onyo la kiakili kwa Umma mzima wa Kiislamu, na iwapo Waislamu wataendelea kutozidi kuwa wamoja, Wazayuni kila mara watazifanya nchi nyingine za Kiislamu kuwa shabaha.
Sayyid Zawar Husayn Naqvi vilevile alitangaza mshikamano wake wa dhati na taifa la Palestina pamoja na uongozi wa muqawama, na akaongeza kusema: Nchi za Kiislamu zinapaswa mara moja kuchukua hatua za pamoja na za kivitendo, na Pakistan kwa kutekeleza wajibu wake wa kihistoria na kiitikadi, ipige hatua ya mwanzo katika kuutetea Umma wa Kiislamu, ili ujumbe ulio wazi uwafikie Israel na wanao waunga mkono.
Maoni yako