Ijumaa 29 Agosti 2025 - 00:29
Shirika la Mawasiliano ya Kiislamu Marekani lakishutumu Chuo Kikuu cha Wayne kwa tabia ya kibaguzi dhidi ya Waislamu

Hawza/ Shirika la Mawasiliano ya Kiislamu Marekani siku ya Jumatatu katika mkutano wake na waandishi wa habari lilitangaza kuwa Chuo Kikuu cha Jimbo la Wayne kinakandamiza na kunyamazisha sauti za Waislamu, Wapalestina na wapinzani wa mauaji ya kimbari

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Bw. Dawud Walid, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano ya Kiislamu Marekani (CAIR), siku ya Jumatatu katika hotuba yake kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mbele ya lango kuu la Chuo Kikuu cha Jimbo la Wayne alisema: “Chuo hiki kinajaribu kukandamiza sauti za watetezi wa haki na wanaounga mkono Palestina, na mara zote kimekuwa kikitafuta njia za kuwatendea Waislamu ubaguzi.”

Walid alisema: “Wanafunzi wanapaswa kuwa na uwezo wa kuzungumza kwa uhuru katika taasisi hii ambayo wanalipa ada ili kusoma, na ambayo inapaswa kuwa mahali salama pa kujifunzia bila upendeleo wowote; pia wasiogope kushughulikia mambo yao ya kimaofisi.”

Aliongeza: “Hii ndiyo desturi yetu hapa Marekani kwamba fikra na habari huwasilishwa kwa uhuru katika maeneo ya umma na kwenye kampasi za vyuo, leo watu wa Ghaza wanakabiliana na baa kubwa la njaa.”

Mmoja wa mawakili wa Shirika la Mawasiliano ya Kiislamu Marekani pia aliwasilisha ripoti kuhusu kunyanyaswa na kutendewa isivyo sawa kwa wanafunzi Waislamu na chuo hicho, moja ya malalamiko hayo yalieleza kwamba; ikiwa mwanafunzi ataenda kuswali msikitini ndani ya chuo, hataruhusiwa tena kurejea kwenye shughuli za masomo au kuendelea na darasa lake, na jambo hilo limepigwa marufuku na uongozi wa chuo.

Mwanafunzi mmoja pia aliongeza kuwa polisi wakati wa mikusanyiko yoyote ya amani huwazuia Waislamu kutumia vipaza sauti, ilhali mikusanyiko mingine yote inaruhusiwa kutumia vipaza sauti na vifaa vingine vya kuongezea sauti.

Chanzo: The Detroit News

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha