Alhamisi 21 Agosti 2025 - 15:45
Shia ni wajuzi wa Uislamu wa kweli

Hawza/ Mtukufu Ayatullah Jawadi Amuli amesisitiza juu ya umuhimu wa nafasi ya Hawza katika kukuza elimu na maarifa kwenye jamii, na akabainisha kuwa: Vitabu kama “Maktab al-Tashayyu’” vinapaswa kuandikwa kwa namna ambayo vizazi mbalimbali, na hata watu wa ulimwengu mzima, waweze kufaidika navyo na kuviona kuwa muongozo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah al-Udhma Jawadi Amuli, siku ya Jumatano tarehe 29 Mordaad, katika kikao na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Kitaaluma, wasimamizi na watafiti wa kitabu “Maktab al-Tashayyu’ kwa riwaya ya Allama Jawadi Amuli,” kwa kubainisha kuwa kitabu kinaweza kuwa cha kimataifa iwapo kimeandikwa na kupangwa kwa mtazamo wa kimataifa, alisema: Uwezo wa Hawza ni mkubwa sana; endapo Hawza itataka, inaweza kutoa matokeo makubwa ya kielimu, kwa mfano, hiki kitabu cha Tafsiri ya Tasnīm ni zao la juhudi ya Hawza, bila shaka kazi hii ni kazi ya Hawza, si kazi ya mtu binafsi, ni matokeo ya baraka za Mapinduzi ya Kiislamu na damu safi ya mashahidi, mimi ni mtu mmoja tu mbele ya kundi hili lenye utukufu, pale darsa hii ilipoanza ilipokelewa kwa hamasa na Hawza na wanazuoni, na ilichukua muda wa vizazi vinne, ambapo vikwazo na shubha za vizazi vinne vilijibiwa na kuondolewa, hivyo, iwapo baadhi ya masuala yametajwa tena na tena, ni kwa kuwa yamehusiana na vizazi vinne.

Ayatulla Jawad alisisitiza juu ya umuhimu wa nafasi ya Hawza katika kukuza elimu na maarifa ya jamii, na akasema: Vitabu kama “Maktab al-Tashayyu’” vinapaswa kuandikwa kwa namna ambayo vizazi mbalimbali ulimwenguni waweze kufaida na kuona kuwa muongozo.

Hadhrat Ayatullah Jawadi Amuli, akielezea nafasi ya Shia ndani ya Uislamu, alisema: Shia kwa hakika siyo dhehebu tu miongoni mwa madhehebu ya Kiislamu, bali ndio Uislamu halisi na wa kweli, Kwa kuwa kutoka mwanzo (mabda’) hadi mwisho (ma’ād) na kutoka ma’ād kurudi mabda’, Shia wana kauli ya kielimu, Shia huzungumza juu ya wajibu na mambo yenye yakini ya kimungu, na suala lake kubwa zaidi la kikalamu ni dharura ya nasbu ya kimungu, hakika Mungu lazima ndiye atakayenasibu (kumweka Imamu), na wajibu huu ni kutoka kwa Mungu, si juu ya Mungu, Kadhalika, Mwenyezi Mungu hakutaka tu kumuumba mwanadamu, bali alimuumba Khalifa wa Mwenyezi Mungu, na akawaamrisha Malaika wasujudu mbele ya Khalifa wa Mwenyezi Mungu, kubainisha masuala haya ya kikalamu kunafafanua njia sahihi ya ufahamu wa dini kwa wanadamu.

Alisisitiza kuwa: Uislamu wa kweli ni ule ambao Shia anauwasilisha, na ufahamu sahihi wa dini hauwezekani bila kuzingatia Uimamu na mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s), Shia kwa kutegemea mafundisho ya Ahlul-Bayt, hunufaika na tafsiri zao na elimu ya akili, na daima hufanya jitihada ya kuyahifadhi hai maarifa ya Qur’ani na dini.

Mtukufu huyo alibainisha: Ufahamu sahihi wa dini na maarifa ya Ahlul-Bayt (a.s), kumtambua Mwenyezi Mungu kwa hakika na kuamini katika Ismah ya Maimamu (a.s), vina nafasi muhimu katika kumuongoza mwanadamu, na Shia ana nafasi ya msingi katika kuyahifadhi na kuyabainisha mafundisho haya.

Huku akiashiria athari za wanazuoni wakubwa wa Hawza, alisisitiza juu ya umuhimu wa kuchunguza kwa makini athari za kielimu na kikalamu, na akabainisha kuwa: Kuchunguza kwa kina na kielimu athari hizi, kunatoa mazingira ya kukua na kupata mwamko wa kidini na kitamaduni kwenye jamii, Ukosoaji wa kielimu na kutolea pingamizi si kizuizi cha maendeleo, bali husababisha ustawi na ukuaji wa kielimu, kila kizazi kinapaswa kwa njia mpya na mbinu mpya, kusoma upya na kuendeleza athari hizi.

Aidha, alikumbushia kwamba kuelewa na kupata elimu si kosa, bali ni jukumu la kwanza la kisheria la kila mwanadamu, kwamba asome na kufahamu maarifa ya dini.

Mtukufu huyo alisisitiza juu ya umuhimu wa kujifunza na kuuliza maswali ya kielimu ndani ya Hawza, na akasema: Shia daima wamejitahidi kuutambulisha Uislamu kwa namna ya kielimu, kikalamu na kivitendo, na wamejitahidi kurahisisha njia ya ukuaji wa kiroho na kiakili kwa wanadamu.

Mwisho, aliwapongeza watafiti wa kitabu “Maktab al-Tashayyu’” na akaonesha matumaini kwamba kazi hii iwe rejea yenye kuaminika kwa vizazi vijavyo, na iwe kielelezo cha ufahamu wa kina wa Uislamu na Ushia.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha