Jumanne 19 Agosti 2025 - 15:51
Jihadharini na wezi wa itikadi

Hawzah/ Ayatullah Ṣāfī Gulpāygānī (ra) alisisitiza kwamba hakuna mali yenye thamani kubwa kuliko “lulu ya akida (itikadi)” kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Mtukufu (saw) na Maimamu watoharifu (as).

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Ṣāfī Gulpāygānī (ra) anaona kwamba kuwa na akida safi kwa Mwenyezi Mungu, Mtume na Maimamu (as) ndiyo lulu na hazina yenye thamani zaidi kwa mwanadamu.

Hakuna lulu wala mali yoyote yenye thamani kubwa na ya thamani kubwa zaidi kuliko lulu ya kuwa na akida sahihi juu ya Mwenyezi Mungu, Mtume na Maimamu (as).

Iwapo mwanadamu ataipoteza dunia na vyote vilivyomo ndani yake lakini akabaki na akida salama juu ya Mwenyezi Mungu na Mtume, hatakuwa na hofu yoyote, lakini iwapo ataikosa akida hiyo, basi chochote alichonacho atakipoteza, maana atakuwa amepata hasara duniani na akhera.

Kwa kuzingatia thamani kubwa ya lulu hii adimu, ndio maana wezi na wahuni wengi wameweka mitego na nyavu za udanganyifu, wakisubiria tu ili waiibe na kuipora akida hiyo.


Chanzo: “Mawaidha ya kupendeza 110 | Kutokana na usia na mawaidha ya Ayatullah Ṣāfī Gulpāygānī (ra)”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha