Jumapili 17 Agosti 2025 - 15:22
Akili Mnemba na Athari Zake katika Mifumo ya Kitamaduni na Kidini

Hawza/ Mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi wa Kidhini (Majlis Khubragān Rahbari) amesisitiza kuwa: kulinda mipaka ya kudiriki ya kijamii dhidi ya uvamizi laini wa adui, kwa kiwango kikubwa ni jukumu la vituo vya kielimu na kitamaduni zikiwemo Hawza za kielimu, katika kifungu cha sita cha ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi katika Arubaini ya Mashahidi wa Izzah, pia imesisitizwa nafasi ya Hawza katika kuongeza basira, kuimarisha na kuleta utulivu katika kijamii.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, kuhusu mustakabali wa akili mnemba, hatua na mikakati katika uwanja huu, tumefanya mazungumzo na Hujjatul-Islam wal-Muslimīn Ali Abbasi, Rais wa Jāmi‘at al-Mustafā al-‘Ālamiyya na Mjumbe wa Majlis Khubragān Rahbari.

Yafuatayo ni maelezi ya mazungumzo hayo:

Swali:
Maoni yenu kuhusu mustakabali wa akili mnemba kutokana na mtazamo wa fikra ya Kiislamu na athari zake zinazowezekana katika mifumo ya kijamii na kidini ni yapi?

Jibu:
Mtazamo wa kimaendeleo kuhusu akili mnemba na athari zake katika mifumo ya kijamii na kidini ni suala lenye pande nyingi, ili kuchambua jambo hili, tunapaswa kuzingatia mambo kadhaa ya kimsingi:

1. Anthropolojia ya Kiislamu:
Katika fikra ya Kiislamu, mwanadamu ni kiumbe mwenye roho, akili na hiari ya uhuru, sasa, akili mnemba ambayo ni kielelezo cha akili ya mwanadamu, inaweza kuibua changamoto juu ya nafasi ya mwanadamu katika ulimwengu, ni lazima kuchunguza iwapo akili bandia inaweza kuhesabiwa kama kiumbe huru au la.


2. Maadili na Wajibu:
Katika Uislamu, jukumu la kimaadili na maamuzi ni la mwanadamu, kwa hivyo, maendeleo ya akili bandia yanapaswa kuzingatia misingi ya maadili ya Kiislamu ikiwemo kuheshimu heshima ya mwanadamu, uadilifu, ukweli na uwajibikaji.


3. Athari za Kijamii na Kidini:
Akili mnemba inaweza kubadilisha miundo ya kijamii, kuanzia soko la ajira, mahusiano ya kijamii, mifumo ya elimu, hadi tabia za kidini, hivyo jamii inapaswa kujiandaa, kupata elimu na kujipanga ipasavyo.


4. Kuzidi kwa Tofauti za Kijamii:
Moja ya hatari kubwa ni ongezeko la pengo la kitabaka kutokana na upatikanaji usio sawa wa teknolojia, katika ngazi ya kitaifa na kimataifa, ikiwa nchi au tabaka fulani tu zitafaidika, basi kutatokea migongano ya kijamii na kimataifa.


5. Athari katika Tafsiri ya Dini:
Moja ya hofu kubwa ni matumizi ya akili mnemba katika uchambuzi wa maandiko ya kidini bila umakini na viwango vya kielimu, inaweza kusababisha upotoshaji wa maana.


6. Mas-ala mapya ya Kifiqhi:
Mas-ali mapya ya kifiqhi yameibuka, kama vile uwajibikaji wa kisheria wa akili mnemba, maamuzi ya kiotomatiki, hifadhi ya faragha na usalama wa kidijitali, haya yanahitaji ijtihād mpya na ya haraka.


7. Fursa:
Kwa upande mwingine, akili mnemba inatoa fursa kubwa kwa taasisi za kidini, ikiwemo kuboresha ubora wa maisha, kurahisisha upatikanaji wa elimu ya dini na kuongeza tija katika huduma za kijamii.

Kwa jumla, mtazamo wa Kiislamu kuhusu akili mnemba unahitaji uchambuzi wa kina ili kuweka mizani kati ya manufaa ya kiteknolojia na ulinzi wa maadili na utu wa mwanadamu.

Swali:
Ni hatua zipi zinapaswa kuchukuliwa katika uwanja wa akili mnemba?

Jibu:

Ili kutumia akili mnemba ipasavyo ndani ya viwango vya Kiislamu na kupunguza changamoto, hatua zifuatazo zinapendekezwa:

۱. Kuendeleza elimu na utafiti wa kiutafiti kati ya fani mbalimbali.

۲. Kubuni algorithimu zenye misingi ya maadili ya Kiislamu.

۳. Kutoa elimu kwa jamii kwa jumla na kuwajengea uwezo.

۴. Mafunzo maalum kwa wanazuoni na watafiti wa kidini.

۵. Kuweka sera na kanuni za kisheria na kimaadili.

۶. Kusimamia na kutathmini mara kwa mara matumizi ya akili bandia.

۷. Kuanzisha majukwaa ya ushirikiano kati ya vyuo na Hawza.

۸. Kukuza utamaduni wa maadili katika teknolojia.

۹. Kufanya mazungumzo ya kimataifa ya kielimu na kidini.

۱۰. Kuweka mazingira ya maendeleo yenye mizani kati ya teknolojia na maadili.

Swali:
Jāmi‘at al-Mustafā imechukua hatua gani za kimsingi katika akili mnemba?

Jibu:

Jāmi‘at al-Mustafā imepanga programu za kuwazoesha wanafunzi, walimu na wasomaji wake kuhusiana na akili bandia na kuwafahamisha juu ya fursa na hatari zake, ili waweze kuitumia katika kazi za kielimu na utafiti.

Swali:
Ni vipengele gani vya kimsingi vilivyotiliwa mkazo na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kuhusiana na akili mnemba?

Jibu:
Kiongozi Mkuu amesisitiza: Kuendeleza miundombinu ya teknolojia ya habari, kulea wataalamu maalum, kusaidia utafiti wa msingi na bunifu, kutunga sera na kanuni za kitaifa, pia ameonya kwamba Iran isibaki mtumiaji pekee wa akili bandia, bali iwe mtengenezaji, vinginevyo utegemezi kwa wageni utahatarisha maslahi na utambulisho wa kitamaduni.

Swali:
Unalitathminije suala la udhibiti wa akili bandia duniani na hatua za Iran?

Jibu:
Tajiriba ya dunia imeonesha kuwa udhibiti wa akili mnemba unahitaji mtazamo wa kina, wa kimaadili na kisheria, mataifa ya Magharibi yameweka kanuni kwa lengo la kulinda maslahi yao na kubakisha ubabe wa kiteknolojia, Iran, kwa upande wake, inapaswa kuchukua mtazamo huru, unaojengwa juu ya utamaduni wa asili.

Swali:
Ni mbinu zipi zinazohitajika kuendeleza diplomasia ya mtandao (cyber diplomacy) kimataifa?

Jibu:
Diplomasia ya mtandao inamaanisha kuimarisha uhusiano wa kidijitali na usalama wa kimtandao kati ya mataifa, hii inahitaji kuendeleza miundombinu ya ICT, ushirikiano wa kimataifa, sera za kitaifa, na kulinda uhuru wa mataifa pamoja na tamaduni zao za asili.

Mwisho wa Ujumbe
 

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha