Jumamosi 2 Agosti 2025 - 09:56
Iran ni kielelezo cha heshima, nguvu, uhuru na kauli ya "Uwe mbali nasi udhalili"

Hawza/ Khatibu wa Swala ya Ijumaa wa Tehran amesema: Ikiwa usitishaji vita utavunjwa, Tel Aviv itasagwasagwa tena, kwa sababu Iran ni kielelezo cha heshima, nguvu, uhuru na kauli ya "Uwe mbali nasi udhalili".

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza Tehran, Ayatollah Khatami, khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran, huku akibainisha kuwa taqwa ni lango la kila toba, alisema: Kwanza, ni lazima tumheshimu Mwenyezi Mungu, na kilele cha kila hekima ni taqwa.

Akaongeza kusema kwamba: Siri na fumbo la mafanikio limo katika kuhifadhi heshima ya Dhati Tukufu ya Rabbani, Katika masuala ya tauhidi yenye umuhimu mkubwa, ni uangalizi maalumu wa Mwenyezi Mungu kwa waumini, wale wanaokuwa na Mungu, Mungu hatowaacha peke yao.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran alibainisha kuwa: Taqwa ni dhana pana sana, na miongoni mwa maneno ya kimaadili ya dini, hakuna neno lililo pana kama taqwa, Taqwa linahusu mipaka yote ya maisha.

Ayatollah Khatami alisisitiza kwamba: Taqwa ya leo ni kuimarisha mfumo wa Kiislamu, na haipaswi kuathiriwa na uvumi.

Akaendelea kusema kuwa: Taqwa ya leo ni utekelezaji wa mikakati saba ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, Katika historia yote, dini imekuwa na gharama, na hakuna wakati ambao udini umekuwa bila gharama, Manabii 40 waliuawa, lakini subira na uvumilivu huambatana na uangalizi wa Mwenyezi Mungu.

Mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi (Majlis Khobregan) alisema: Adui anataka kuwavunja watu moyo, lakini Qur’an inasema, vumilieni na mtatazama ladha tamu ya ushindi.

Ayatollah Khatami, akisisitiza kuwa kuwaheshimu Ahlul-Bayt ni mhimili wa umoja, alisema: Katika ulinzi wa siku 12, lazima tuelewe ni nani mshindi na ni nani aliyeshindwa. Kwa sababu 11, nasema mshindi wa uwanja huu ilikuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na aliyeshindwa alikuwa utawala wa Kizayuni, bila shaka, vita vina gharama; tumepoteza makamanda wakubwa kama vile Shahidi Baqeri, Shahidi Salami, Shahidi Rashid na wanasayansi wa nyuklia, lakini vilevile adui alipata majeraha makubwa.

Akaendelea kusema kuwa: Adui daima amekuwa akitafuta kutuangamiza sisi, Sasa wanazungumzia maangamizi kwa sababu wanaona wapo katika hali ya mauti na maisha, lakini sisi tumesimama imara.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran alibainisha kuwa: Walitaka tusiwepo, lakini kwa upofu wa macho yao, tumebaki na tutabaki, na tutawafikisha katika hali ya fedheha.

Mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi akaongeza kwa kusema: Pili, maandamano katika nchi mbalimbali yanaonesha chuki dhidi ya Israel. Kinyume chake, Iran imekuwa tukufu na imeonesha nguvu zake, baada ya Vita vya Pili vya Dunia, kwa mara ya kwanza, nchi moja kwa ujasiri ilishambulia kituo cha Marekani, Iran kwa nguvu ilishambulia kituo cha Al-Udeid na kuonesha nguvu zake ulimwenguni.

Akaendelea kwa kusema: Tatu, katika jinai hii ilidhihirika kuwa utawala wa Kizayuni ni kidonda cha saratani, na dunia inapaswa kuondoa kidonda hiki haraka iwezekanavyo.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran akizihutubia nchi za Kiislamu alisema: Kama utawala huu utapata nguvu, balaa lilelile waliloliweka juu ya Syria watalileta juu yenu, Iran ya Kiislamu haikuanzisha vita, bali ilijilinda kwa moyo wote.

Ayatollah Khatami alibainisha: Ikiwa usitishaji vita utavunjwa, Tel Aviv itasagwasagwa tena, katika shambulizi hili, heshima na hadhi ya demokrasia ya kiliberali ya Magharibi ilikwenda, Demokrasia ya kiliberali ya Magharibi imekuwa mauaji ya watoto, mauaji ya wenye njaa na kiu, na wanawake wajawazito, katika siku hizi 12, kinyume cha udini kimeongezeka zaidi, Iran ni kielelezo cha heshima, nguvu, uhuru na kauli ya "Uwe mbali nasi udhalili".

Mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi akaongeza: Kujiingiza moja kwa moja kwa Marekani vitani kulikuwa kwa ajili ya kuokoa utawala wa Kizayuni, dunia inaelewa vizuri kwa nini kauli ya "kifo kwa Marekani" haiondoki midomoni mwa watu.

Akaendelea kwa kusema kwamba: Chuki ya wananchi wetu wapendwa dhidi ya utawala wa Kizayuni na Marekani imeongezeka zaidi, ikiwa siku zile tusingelikubali, baadhi ya watu wa ndani wangesema; nchi imejiingiza vitani; lakini sasa hoja imekamilika na chuki hii inaendelea kuongezeka.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran alisema: Magharibi ilidhani kwamba kwa kuanzisha vita, ghasia zitatokea ndani ya Iran, lakini taifa la Iran limekuwa thabiti na limeungana zaidi kuliko zamani.

Akaelezea zaidi: Nchi za Magharibi na Marekani zote zimesimama upande wa utawala huu, lakini upendo kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi umeongezeka, na kauli ya "damu iliyomo mishipani mwetu ni zawadi kwa kiongozi wetu" imekuwa na nguvu zaidi.

Ayatollah Khatami alisema kwamba: Wamekiri kwamba wanalenga kuangamiza mfumo, na wanaendelea kurudia upuuzi huu, lakini imani ya watu kwa uongozi na vikosi vya ulinzi imeongezeka.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran akaongeza kwa kusema: Kwa juhudi za vikosi vyetu vya ulinzi, Tel Aviv na Haifa zimegeuka kuwa miji ya mizimu. Utawala katika vita vya kisaikolojia ulitaka kuwaogopesha watu na kuwaonesha wakiwa wamechoka, wasijue kwamba watu hawajaathirika na vitisho hivi, na watakabiliana na uchovu kwa uchovu,  amesema: Kwa matokeo ya ulinzi wa kishujaa wa vikosi vyetu vya ulinzi, watu wengi nchini Israel walichagua kukimbia badala ya kubaki, upuuzi huu mlioufanya unaonesha balaa lililowapata; lakini mkijaribu tena, operesheni ya kuwasambaratisha itamiminika juu yenu.

Mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi ameongeza kuwa: Tarehe 15 Mordad (Agosti 6) ni kumbukumbu ya shambulio la bomu la nyuklia dhidi ya Japani, vita vilikuwa vimeisha, lakini Magharibi, kwa ajili ya kujaribu silaha zake za nyuklia, ilifanya shambulio la kinyuklia na kuua watu 160,000.

Amesisitiza kuwa: Marekani katika miaka ya hivi karibuni imevamia nchi 25 duniani, moja kwa moja na kwa njia isiyo ya moja kwa moja, rekodi ya Marekani ni nyeusi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha