Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Sayyid Shujaʿat Ali Kazimi, msemaji wa Baraza la Mawasiliano la Jaʿfariyya 'Azad Kashmir Pakistan, kupitia tamko rasmi, ametoa jibu kali kufuatia kufunguliwa kwa kesi bandia dhidi ya wahubiri wa Kishia katika eneo la Muzaffarabad, na ametaja hatua hiyo kuwa ni uchochezi, ukosefu wa haki, na kinyume na misingi ya kisheria na haki za uraia.
Katika tamko hilo imesisitizwa kuwa: Malalamiko yaliyowasilishwa yameandaliwa bila kuchunguzwa kwa kina maudhui ya hotuba, bila kusikiliza mtazamo wa Madhehebu ya Ahlul-Bayt (as), na bila kurejea vyanzo sahihi vya Kishia na Kisunni kuhusu sababu ya kushuka kwa aya za Qur’ani na tafsiri zake. Hatua hizi zimechukuliwa kwa mashinikizo ya baadhi ya harakati za misimamo mikali na zenye lengo la kuchochea mifarakano ya kidini. Vitendo hivi si tu vinapingana na misingi ya Katiba, bali vinaongeza hali ya mvutano na tofauti za kidini katika eneo hili.
Maoni yako