Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei ametoa jibu kwa swali la kifiqhi kuhusu “swala na funga kwa wanafunzi wa hawza na vyuo vikuu katika miji wanayosomea,” ambalo linawasilishwa kwa wapenzi wa masuala haya kama ifuatavyo:
Swali:
Watu wanaokaa katika mji mwingine tofauti na mji wao wa asili kwa ajili ya kazi, masomo na mambo mengine yanayofanana, kwa muda wa kiasi cha kutosha; je, swala yao katika mji huo inakuwa kamili au wanapaswa kuiswali kwa kufupisha (qasr)?
Jawabu:
Iwapo mtu ananuia kukaa katika mji huo kwa muda wa mwaka mmoja au zaidi kwa namna ambayo kijamii (kwa mtazamo wa kawaida wa watu) hahesabiwi tena kuwa msafiri, basi swala katika mji huo itaswaliwa kikamilifu katika hali yoyote ile, na funga yake ni sahihi, na hatakuwa na haja ya kunuia kukaa siku kumi.
Maoni yako