Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Michigan nchini Marekani waliokuwa wakishiriki kwenye maandamano ya kuiunga mkono Palestina na watu wa Ghaza, wamesema kupitia mahojiano mbalimbali kwamba chuo hicho kimewaajiri watu ili kuwafuatilia, kuwachukua video na picha, kurekodi mazungumzo yao ya kila siku, na kuwapeleleza. Upelelezi huo unafanyika si tu ndani ya chuo, bali hata nje ya chuo pia unaendelea.
Kwa mujibu wa gazeti la "The Guardian" la Uingereza, wanafunzi waliokuwa wakipinga hatua hiyo pia wameeleza kuwa upelelezi na udhibiti huo umefikia kiwango cha kuwa mbinu ya unyanyasaji na vitisho.
Maoni yako