Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, katika matamshi yake huku akigusia migogoro inayoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, alitoa wito wa kuheshimiwa kwa mamlaka ya nchi, kusitishwa kwa mapigano, na kuungwa mkono mchakato wa amani na uthabiti.
Guterres, akisisitiza ukali wa janga la kibinadamu katika Ukanda wa Ghaza, alibainisha kuwa: “Hakuna uhalali wowote wa kuwatesa na kuwafukuza watu wa Palestina. Tunaukosoa vikali muendelezo wa kuwafukuza watu wa Ghaza.”
Maoni yako