Alhamisi 1 Mei 2025 - 07:50
Wanazuoni wakubwa wamechukua baraka za elimu walizonazo na uchamungu kutoka kwa Hadhrat Ma‘suma (s.a)

Haramu ya Hadhrat Ma‘suma ni haramu yenye rehema na fadhila, wanazuoni wakubwa wameusia kwamba muwapo Qum, muanze kwa kutawasali kutoka kwa bi bi Hadhrat Ma‘suma (s.a).

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Hadhrat Ayatollah Jawadi Amuli katika kikao chake cha darsa ya Fiqhi, sambamba na kuiheshimu siku ya kuzaliwa Hadhrat Fatima Ma‘suma (Salamullahi ‘alayha), alieleza:
Mwanamke katika Uislamu si mtu wa kawaida tu, sio wanawake wote ni sawa, wala wanaume wote si sawa. Tazameni bibi huyu mkubwa (Hadhrat Ma‘suma Salamullahi ‘alayha); angalau Ma’sumin watatu wameonyesha heshima maalumu kwake. Daraja yake ni ya juu kiasi kwamba Imam Ma‘sūm amemwandikia Ziyārah maalumu, Ziyārah ambayo inaonyesha mapenzi kwake: “Salamu juu ya binti wa Imam, salamu juu ya dada wa Imam, salamu juu ya shangazi wa Imam.” Mahusiano haya yote ni dalili ya ukubwa wa daraja ya bibi huyo.

Mtukufu huyo aliendelea, huku akiashiria baraka za kuwa karibu na kaburi la Hadhrat Ma‘suma Salamullahi ‘alayha, na kubainisha: Bibi huyu mkubwa ni bibi wa daraja la juu sana, na alama ya cheo chake kikubwa ni hii Hawza ya Qum yenye baraka, ambayo ilianzishwa kando ya kaburi lake lenye nuru. Shughuli nyingi za kielimu, ikiwa ni pamoja na Fiqhi, zilianza kando ya kaburi hili tukufu.

Wao, kwa kusisitiza juu ya nafasi ya kiroho ya haramu ya Hadhrat Ma‘suma Salamullahi ‘alayha, walieleza: Haramu ya Hadhrat Ma‘suma Salamullahi ‘alayha ni haramu ya rehema na fadhila. Wanazuoni wamependekeza kuwa muwapo Qum, muanze kwa kumtaka msaada Bi Bi Hadhrat Ma‘suma Salamullahi ‘alayha; bibi ambaye amefikia kilele cha ukaribu na Mwenyezi Mungu, kiasi kwamba Ma‘sumin watatu (Alayhimus Salaam) wamempa salamu kutokana na daraja lake. Kando ya kaburi tukufu la bibi huyu mkubwa, wamelala wanazuoni na mar'aj'i wakubwa, ambao uwepo wao ni chanzo cha baraka.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha