Jumanne 22 Aprili 2025 - 17:46
Sifa za Imam: "Kuisimamia jamii na Kupambika katika maadili yaliyo kamilika"

Imam, ambaye ni kiongozi na muongozaji wa jamii, ni lazima ajiepushe na maovu yote pamoja na tabia potofu kimaadili, na badala yake awe ni mwenye sifa zote bora na maadili ya kiwango cha juu kabisa, kwa sababu kama yeye atakuwa mtu mkamilifu, basi atachukuliwa kuwa kielelezo bora zaidi kwa wafuasi wake.

Kwa mujibu wa s Shirika la Habari la Hawza | Miongoni mwa sifa muhimu za Imam na masharti ya msingi ya Uimamu ni: (Kuisimamia jamii na Kupambika katika maadili yaliyo kamilika).

Kuisimamia jamii:
  
Kwa kuwa mwanadamu ni kiumbe wa kijamii, na jamii ina athari kubwa katika nafsi, akili na mwenendo wake, basi ni lazima mazingira ya kijamii yaliyo mwafaka yaandaliwe ili kumlea na kumkuza ipasavyo kuelekea kumkurubia Mwenyezimungu, na hili linawezekana chini ya uundwaji wa serikali ya kimungu. Kwa hivyo, Imam ambaye ni kiongozi wa watu, ni lazima awe na uwezo wa kuendesha mambo ya jamii, na kwa kutumia mafundisho ya Qur'ani na Sunna ya Mtume pamoja na kuwashirikisha watu wenye uwezo, aanzishe utawala wa Kiislamu.

 Kujipamba Imamu na ukamilifu wa maadili:
  
Imam ambaye ni kiongozi na muongozaji wa jamii, ni lazima ajiepushe na maovu yote ya kimaadili, na badala yake awe ni mwenye kumiliki fadhila zote bora za kimaadili kwa kiwango cha juu kabisa, hii ni kwa sababu tu, endapo yeye kama akiwa ni mtu mkamilifu, basi atakuwa ni mfano bora zaidi kwa wafuasi wake.

Imam Ridha (a.s) anasema kuhusiana na hili:

«لِلْإِمَامِ عَلاَمَاتٌ یَکُونُ أَعْلَمَ النَّاسِ وَ أَحْکَمَ النَّاسِ وَ أَتْقَی النَّاسِ وَ أَحْلَمَ النَّاسِ وَ أَشْجَعَ النَّاسِ وَ أَسْخَی النَّاسِ وَ أَعْبَدَ النَّاسِ.»

“Imam ana alama: Yeye ndiye mwenye elimu zaidi miongoni mwa watu, mwenye busara zaidi, mcha Mungu zaidi, mvumilivu zaidi, shujaa zaidi, mkarimu zaidi, na mcha Mungu zaidi miongoni mwa watu.” (Al-Khisal, ju. 2, uk. 527)

Aidha, kwa kuwa Imam (a.s) anashikilia nafasi ya khalifa wa Mtume (s.a.w), anawadhifa wa kulea na kuelimisha wanadamu. Hivyo basi, yeye mwenyewe anapaswa kuwa amepambika na maadili ya kimungu zaidi kulikoa watu wengine wote.

Imam Ali (a.s) anasema kuhusiana na kadhia hii:

«مَنْ نَصَبَ نَفْسَهُ لِلنَّاسِ إِمَاماً، [فَعَلَیْهِ أَنْ یَبْدَأَ] فَلْیَبْدَأْ بِتَعْلِیمِ نَفْسِهِ قَبْلَ تَعْلِیمِ غَیْرِهِ؛ وَلْیَکُنْ تَأْدِیبُهُ بِسِیرَتِهِ قَبْلَ تَأْدِیبِهِ بِلِسَانِهِ.»

“Yeyote anayejinasibisha kuwa Imam wa watu, basi ni wajibu kwake aanze kujielimisha mwenyewe kabla ya kuwaelimisha watu wengine, na awafundishe watu kwa mwenendo wake kabla ya kuwaelimisha kwa maneno yake.” (Nahj al-Balaghah, Hekimah no. 73)

Utafiti huu unaendelea…

Imenukuliwa kutoka katika kitabu kiitwacho “Nengin Afarinesh”, pamoja na kufanyiwa mabadiliko kiasi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha