Jumapili 13 Aprili 2025 - 18:45
Ayatollah al-udhma Jawadi Amuli ameuliza: Je! Ziara ya Amirul mu’uminin (a.s.) ni bora zaidi au ziara Imamu Hussein (a.s.)?

Hadhrat Ayatollah al-udhma Jawadi Amuli, kwa kurejea riwaya kutoka kwa Imamu Kadhim (a.s.), ameeleza bayana: Imamu alisema, "Yeyote atakayekubali wilaya ya wa kwanza miongoni mwetu, amekubali wilaya ya wa mwisho wetu; kama ambavyo akubaliye wilaya ya wa mwisho wetu, basi amekubali wilaya ya wa kwanza wetu."

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hadhrat Ayatollah Jawadi Amuli katika maandiko yake akizungumzia mada ya kipi ni bora zaidi kati ya ziara ya Amirul Mu’uminin (a.s) au ziara ya Imamu Hussein (a.s), kwa kurejea riwaya kutoka kwa Imamu Kadhim (a.s.), alisisitiza kuwa:

Abdulrahman bin Muslim alimuuliza Imamu Kadhim (a.s) na akasema: Je, ziara ya Amirul Mu’uminin (a.s) ni bora zaidi au ziara ya Imamu Hussein (a.s) au ziara ya fulani miongoni mwa maimamu, na akawataja mmoja baada ya mwingine.

Imamu Kadhim (a.s) alimjibu:

“Ewe Abdulrahman! Yeyote atakayemzuru wa kwanza wetu, basi amemzuru wa mwisho wetu; kama ambavyo atakayemzuru wa mwisho wetu, basi amemzuru wa kwanza wetu. Yeyote atakayekubali uongozi wa wa kwanza wetu, basi amekubali uongozi wa wa mwisho wetu, kama ambavyo akubaliye uongozi wa wa mwisho wetu, basi amekubali uongozi wa wa kwanza wetu. Na yeyote atakayetimiza haja ya mmoja wa wapenzi wetu, ni kana kwamba ametimiza haja zetu sisi sote.”

Rejea: Bihar al-Anwar, juzuu ya 97, ukurasa wa 122.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha