Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, hadhrat Ayatollah Ali Khamenei ametoa jibu la swali lililohusu “hukumu ya mtoto kugusa Qur'ani,” jawabu lake nalo ni kama ifuatavyo.
Kugusa Qur'ani Mtoto mdogo
Swali:
Ikiwa mtoto atafungua Qur'ani na kugusa aya kwa mkono wake, sisi tunapaswa kufanya nini? Je, ni lazima tumchukue Qur'ani japokuwa kufanya hivyo kutamfanya alie?
Jawabu:
Kugusa maandiko ya Qur'ani si haramu kwa mtoto, na si wajibu kwa waliobaleghe kumzuia mtoto asiguse maandiko ya Qur'ani.
Maoni yako