Jumapili 6 Aprili 2025 - 17:47
Kuzuiwa wanafunzi wanaounga mkono Palestina katika vyuo vikuu vya Uingereza

Maria Ali na Antonia Listert, ni wanafunzi wawili kutoka chuo kikuu cha Birmingham Uingereza, walikutana na mashitaka ya nidhamu kwa sababu ya kuunga mkono watu wa Ghaza na kulaani vitendo vinavyo fanywa na utawala haramu wa kizayuni.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika Shirika la Habari la Hawza, wanafunzi hawa walikiomba chuo chao kuacha kuwekeza katika makampuni yanayotoa silaha kwa utawala wa kizayuni.

Matukio ya ubaguzi dhidi ya wanafunzi wanaounga mkono Palestina katika vyuo vikuu vya Uingereza, yamezusha wasiwasi mkubwa miongoni mwa mashirika ya haki za binadamu na wataalamu wa kimataifa.

Ni muhimu kutambua kuwa sera hizi za ukandamizaji, zinafanyika wakati ambao katika miezi ya hivi karibuni kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la matukio kama haya dhidi ya wanafunzi na wanaharakati wanaounga mkono Palestina, katika vyuo vikuu mbalimbali barani Ulaya na Marekani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha