Jumamosi 29 Machi 2025 - 13:30
Ununuzi na uuzaji Noti

Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi alijibu swali kuhusu "Ununuzi na uuzaji wa Noti".

Kulingana na ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Hadhrat Ayatollah Khamenei alijibu swali kuhusu "Ununuzi na uuzaji wa Noti," na jibu lake ni kama ifuatavyo.

Swali: Ununuzi na uuzaji wa Noti kwa mkopo, kwa kiasi kikubwa kuliko thamani yake, kuna hukumu gani?

Jibu: Ikiwa biashara hiyo inafanywa kwa nia ya dhati na kwa lengo linaloingia akilini, kama vile ambavyo Noti hizo zitatofautiana (kama vile mpya au za zamani), au kama zitakuwa na alama maalum, au zitatofautiana bei, hakuna shida. Lakini ikiwa biashara hiyo ni ya kisanii tu na inalenga kuepuka riba hali ya kuwa kiuhalisia inalenga kupata faida kutokana na fedha, kisheria ni haramu na batili.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha