Jumamosi 29 Machi 2025 - 13:20
Matembezi ya mwaka huu ni miongoni mwa matembezi bora zaidi, yaliyo na heshima na utukufu zaidi kuliko matembezi mengine yaliyowahi kufanyika katika Siku ya Quds

Hawaza: Kiongozi wa Mapinduzi ya kiislamu, Hadhrat Ayatollah Khamenei, alisisitiza katika ujumbe wake wa televisheni usiku huu kuwa, matembezi ya mwaka huu ya Siku ya Quds ni muhimu zaidi kuliko miaka iliyo pita, na kusema: "Insha'Allah, matembezi ya mwaka huu yatakuwa mojawapo ya matembezi bora, yenye heshima na ya fahari zaidi kuwahi kutokea katika matembezi ya siku ya Quds."

Kwa mujibu wa ripoti kutoka katika Shirika la Habari la Hawza, katika ujumbe wake usiku wa leo, Hadhrat Ayatollah Khamenei, kiongozi wa Mapinduzi ya kiislamu, alieleza kuwa; Insha'Allah, matembezi ya mwaka huu yatakuwa mojawapo ya matembezi bora, yenye heshima na ya fahari zaidi kuwahi kutokea katika matembezi ya Siku ya Quds."

 Kiongozi wa Mapinduzi katika ujumbe wake aliashiria kuwa matembezi ya Siku ya Quds ni alama ya umoja na nguvu ya taifa la Iran, na kusema: "Matembezi haya pia ni alama ya kuwa taifa la Iran limesimama imara katika malengo yake muhimu na ya kisiasa, na kamwe halitaacha msimano wake wa kuitete na kuikingia kifua Palestina."

Hadhrat Ayatollah Khamenei alisema kuwa: Matembezi ya Siku ya Quds ni fahari kwa taifa la Iran: Taifa la Iran limekuwa likishiriki katika matembezi ya Siku ya Quds kwa miaka arobaini na sita sasa, huku wananchi wake wakiwa wamefunga na hata katika hali ya hewa tofauti, na ushiriki huu haukufanyika tu katika miji mikubwa, bali pia katika miji midogo na vijiji.

Aliongeza kusema kuwa umuhimu wa Siku ya Quds mwaka huu ni mkubwa zaidi kuliko miaka iliyopita, na kusema: "Mataifa mbali mbali duniani na wale wanaofahamu mfumo wa kiislamu wanaiunga mkono Iran, lakini baadhi ya sera za serikali zinazoipinga Jamhuri ya Kiislamu zinajaribu kutangaza kuwa kuna mgawanyiko na udhaifu kati ya watu wa Iran kwa kupitia matangazo yao ya uongo, lakini matembezi ya Siku ya Quds yatabatilisha maneno hayo yasiyo na msingi."

Mwisho, Kiongozi wa Mapinduzi ya kiislamu alionyesha matumaini yake kuwa, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, matembezi ya Siku ya Quds mwaka huu yatakuwa mojawapo ya matembezi bora, yenye heshima na ya fahari zaidi kuliko matembezi ya miaka ya hivi karibuni.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha