Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, tamko la Baraza la Uratibu la Taasisi za Hawza kuhusu Siku ya Kupambana na Ubeberu wa Kimataifa, ambalo limesainiwa na Ayatullah A'rafi, Mwenyekiti wa Baraza la Uratibu la Taasisi za Hawza, linasema kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
«Na hakika Mwenyezi Mungu atamnusuru yule anayemnusuru Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.»
Imam Khomeini (r.a.) amesema: “Marekani na Israel ni maadui wa msingi wa Uislamu, kwa sababu wanaiona dini ya Uislamu, Kitabu chake na Sunna yake kuwa ni kikwazo katika njia yao na kizuizi dhidi ya uporaji wao. Hii ni kwa sababu Iran, kwa kufuata Kitabu hicho na Sunna hiyo hiyo, iliweza kusimama dhidi yao, kufanya mapinduzi na hatimaye kupata ushindi.”
Tarehe 13 Aban, ambayo ni Siku ya Kitaifa ya Kupambana na Ubeberu wa Kimataifa, ni fursa ya kihistoria ya kuhuisha fikra na misingi ya kupinga ubeberu pamoja na kuisikika kwa nguvu kaulimbiu ya “Kifo kwa Marekani”.
Siku hii inaambatana na matukio matatu muhimu ya kihistoria yaliyotokea katika miaka ya 1343 (1964), ambapo Imam Khomeini (r.a.) alihamishwa kwa lazima kwenda Uturuki; mwaka 1357 (1978), ambapo wanafunzi wa shule waliuawa kikatili; na mwaka 1358 (1979), ambapo jengo la ujasusi la Marekani lilitekwa.
Kutokana na matukio hayo, siku hii imekuwa alama ya heshima, mapambano, kuwadhoofisha maadui na kupinga ubeberu kwa taifa la Iran, huku ikiwa ni ishara ya kushindwa, fedheha na udhalilifu kwa maadui wa nchi hiyo.
Leo, kwa rehema za Mwenyezi Mungu, mataifa yaliyodhulumiwa na yaliyowekwa chini ya utawala wa ubeberu wa kimataifa na Israel mporaji, hususan Palestina yetu pendwa, yameamka kwa kuiga mapinduzi adhimu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Mataifa hayo yameanzisha harakati kubwa kwa lengo la kujitwalia hatima yao wenyewe, kuuangusha mfumo wa utawala wa kibeberu na kuanzisha mfumo mpya wa dunia.
Muqawama wa kishujaa uliojaa msimamo thabiti na kujitolea muhanga kwa wananchi na wapiganaji wa Palestina umeandika ukurasa wa dhahabu katika historia ya Uislamu na historia ya zama hizi. Aidha, kwa mara nyingine umeionyesha dunia utukufu na adhama ya Uislamu na Waislamu, ambayo msingi wake ni imani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Hali hii inathibitisha yale aliyoyasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur’ani Tukufu:
«Wala msilegee wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio mtakaokuwa juu ikiwa nyinyi ni Waumini.»
(Surat Aal-Imran, Aya ya 139).
Kwa upande wake, Hawza huku zikihifadhi kumbukumbu na kuenzi historia ya Imam Khomeini (r.a.), pamoja na ushujaa na kujitoa muhanga mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu na wananchi wote wenye uelewa wa Iran katika medani za mapambano dhidi ya Marekani na ubeberu wa kimataifa, zimesisitiza umuhimu wa Muqawama wa mataifa ya Kiislamu dhidi ya Marekani na Israel mporaji, pamoja na kushikamana na malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu kwa kufuata maelekezo na mwongozo wa Imam Khamenei (Mwenyezi Mungu amuhifadhi).
Vilevile, Hawza hizo zinatoa wito kwa wananchi wote wa Iran, hususan wanafunzi wa Hawza, wanafunzi wa vyuo vikuu na wanafunzi wa shule, kushiriki kwa hamasa kubwa na moyo wa kimapinduzi katika hafla za kuadhimisha Siku ya 13 Aban.
Kupitia ushiriki huo na kulaani jinai za Marekani, Israel na ubeberu wa kimataifa, wanapaswa kuwakatisha tamaa maadui wa Uislamu na kuwasha tena mwanga wa matumaini katika nyoyo za wanyonge na wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.
Vilevile, viongozi wote wa dini, wanafunzi wa Hawza, wanazuoni pamoja na wananchi wa kimapinduzi wa Qum wanaalikwa kushiriki kwa wingi na kwa nguvu katika hafla kubwa ya kuadhimisha Siku ya Mwenyezi Mungu, tarehe 13 Aban, itakayofanyika katika Haram Tukufu ya Bibi Fatimah Maasumah (s.a.), ili kwa mara nyingine wapige pigo kali katika kinywa cha ubeberu wa kimataifa na utawala wa Israel muuaji.
Ayatullah Alireza A'rafi
Mwenyekiti wa Baraza la Uratibu la Taasisi za Hawza
Maoni yako