Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, programu hiyo ilifanyika katika mazingira yaliyojaa imani, pamoja na kudhihirisha mapenzi juu ya Ahlul-Bayt (a.s.), ambapo waumini walipata fursa ya kukusanyika pamoja kwa ajili ya kukumbuka maisha na utukufu wa Bibi Zainab (s.a.), ambaye anajulikana kwa subira yake, ujasiri wake na msimamo wake thabiti katika kulinda mafundisho ya Uislamu.
Katika sehemu ya kwanza ya programu hiyo, ilisomwa Hadith al-Kisa, kisha khutba na baadaye, waumini walifuatilia qaswida mbalimbali zilizotolewa kwa lengo la kuwasifu na kuadhimisha fadhila za Ahlul-Bayt (a.s.), katika hali iliyoongeza hamasa na kuimarisha mshikamano.
Maadhimisho hayo yalikuwa pia fursa ya kuwakumbusha waumini umuhimu wa kujifunza kutokana na mwenendo wa Bibi Zainab (s.a.), hususan katika nyanja za ujasiri, subira, uimara wa imani na kusimama imara katika kutetea haki. Maisha yake yanaendelea kuwa mfano muhimu kwa Waislamu katika kukabiliana na changamoto mbalimbali huku wakishikamana na misingi ya dini yao.



Maoni yako