Jumatano 23 Septemba 2026 - 01:02
Ayatullah al-Udhma Shubayri Zanjani amemaliza karne nzima pamoja na Qur’ani, Ahlul-Bayt na kuwaongoza watu

Hawza/ Ayatullah Jawadi Amuli ametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Ayatullah Shubayri Zanjani (ra), miongoni mwa Maraji' wakuu wa taqlidi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Jawadi Amuli ametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Ayatullah Shubayri Zanjani, miongoni mwa Maraji' wakuu wa taqlidi.

Maandishi ya ujumbe wa Ayatullah Jawadi Amuli ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَیْهِ رَاجِعُونَ

Hakika kufariki dunia Marji' mwenye hadhi kubwa, Ayatullah al-Udhma Shubayri Zanjani, ni msiba wenye kuhuzunisha kwa dini na utamaduni.

Alikuwa mwanazuoni mashuhuri wa fiqhi ambaye alifahamu nguzo za msingi za fiqhi ya Imamiya, akawalea na kuwaandaa wanazuoni wenye nafasi muhimu na walimu watakaodumu, na akaandika vitabu vyenye thamani kubwa; na akaitumia karne nzima ya maisha yake pamoja na Qur’ani, Ahlul-Bayt na kuwaongoza watu.

وَسَلَامٌ عَلَیْهِ یَوْمَ وُلِدَ وَیَوْمَ یَمُوتُ وَیَوْمَ یُبْعَثُ حَیًّا

Mwisho wa ujumbe

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha