Jumanne 22 Septemba 2026 - 13:32
Ayatullah Al-Udhma Wahid Khorasani Atoa Salamu za Rambirambi Kufuatia Kifo cha Ayatullah Al-Udhma Shubairi Zanjani

Ujumbe wa rambirambi wa Ayatullah Al-Udhma Wahid Khorasani kufuatia kufariki dunia Ayatullah Al-Udhma Shubairi Zanjani umewasilishwa kwa familia ya Marji' huyo wa Taqliid.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kufuatia kufariki dunia Ayatullah Shubairi Zanjani, asubuhi ya leo mtoto mkubwa wa Ayatullah Wahid Khorasani alifika katika ofisi ya Marji' huyo aliyefariki dunia, na kuufikisha ujumbe wa rambirambi wa Ayatullah Wahid Khorasani kwa familia na waliobaki nyuma yake.

Katika ujumbe huo, Ayatullah Al-Udhma Wahid Khorasani alieleza kwamba; kumpoteza Ayatullah Shubairi Zanjani ni msiba mkubwa Hawza. Aidha, sambamba na kutoa salamu za rambirambi kufuatia kufariki dunia Marji' huyo mtukufu, alimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amjaalie marehemu huyo awe pamoja na Amirul-Muuminina Ali (a.s.), na kwa watoto wake watukufu pamoja na ndugu na jamaa wote waliobaki nyuma yake, akamuomba Mwenyezi Mungu awajaalie subira njema na malipo makubwa.

Ayatullah Al-Udhma Wahid Khorasani Atoa Salamu za Rambirambi Kufuatia Kifo cha Ayatullah Al-Udhma Shubairi Zanjani

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha