Jumamosi 12 Septemba 2026 - 22:30
Ujenzi wa makaburi ya Kiislamu nchini Scotland

Hawzah/ Taasisi moja ya hisani kwa kushirikiana na Waislamu wa Scotland, inapanga kujenga makaburi ya Kiislamu nchini humo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, taasisi ya hisani iitwayo Wafaa inajitahidi kujenga makaburi ya Kiislamu katika eneo la Midlothian, nchini Scotland, na kuwezesha utoaji wa huduma za kuisaidia jamii pamoja na maziko ya miili Waislamu wanaofariki dunia.

Ardhi hiyo kwa sasa inamilikiwa na Lothian Estates, na iwapo mpango huo utaidhinishwa inatarajiwa kwamba umiliki wake utahamishiwa kwa Wafaa Foundation.

Mapendekezo hayo pia yanajumuisha ujenzi wa majengo mawili ya mazishi kwa ajili ya kusimamia shughuli za maziko, pamoja na kujengwa chumba kipya cha kuoshea maiti na eneo la maegesho ya magari.

Ombi hilo kwa sasa linachunguzwa na Baraza la Midlothian, ambalo litaamua iwapo mradi huo wa makaburi unaweza kuendelea au la.

Chanzo: tfn.scot

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha