Alhamisi 20 Agosti 2026 - 12:50
Hatari ya dhambi ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja; kutoka kusahau maumbile ya asili hadi kubadilika kwa neema

Hawzah/ Kukaidi njia ya maumbile ya asili aliyoyaweka Mwenyezi Mungu humtoa mtu katika hali inayokusudiwa ya neema za Mwenyezi Mungu; na kugeuza “mvua ya rehema” kuwa “mawe ya adhabu”; taswira inayomwita mwanadamu kutafakari juu ya madhara ya dhambi, kurejea katika maumbile ya asili aliyoyaweka Mwenyezi Mungu, na kuomba msamaha na rehema za Mwenyezi Mungu.

Shirika la Habari la Hawza | Mwanadamu mwanzoni mwa uumbwaji wake huwa kama chombo kitupu, lakini kilicho tayari kupokea athari za mila na desturi, fikra na maadili mbalimbali katika kipindi cha maisha yake, yawe ya haki au batili. Mifumo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii nayo ina nafasi katika kuunda mtazamo na shakhsia yake. Pamoja na hayo, Mwenyezi Mungu ameweka ndani ya mwanadamu maumbile ya asili ya kiungu (fitra) na mwelekeo wa ndani wa kuitambua haki na kuifuata, ili aweze kutambua njia ya ukweli miongoni mwa athari mbalimbali za mazingira na kuifuata; kama Mwenyezi Mungu Mtukufu anavyoashiria ukweli huu katika Qur’ani Tukufu:

«فَأَقِمْ وَجْهَکَ لِلدِّینِ حَنِیفًا فِطْرَتَ اللَّهِ الَّتِی فَطَرَ النَّاسَ عَلَیْهَا لَا تَبْدِیلَ لِخَلْقِ اللَّهِ ذَٰلِکَ الدِّینُ الْقَیِّمُ وَلَٰکِنَّ أَکْثَرَ النَّاسِ لَا یَعْلَمُونَ.»

“Basi elekeza uso wako katika dini ya kweli kwa unyofu. Hayo ndiyo maumbile ya Mwenyezi Mungu ambayo amewaumba watu juu yake. Hakuna mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo dini iliyo nyoofu, lakini watu wengi hawajui.”

(Rum/ 30)

Wakati mwingine uzembe na kutokuwa na ufahamu humtawala mwanadamu kiasi kwamba husahau ukweli wa maumbile yake ya asili ya kiungu, na kwa uchaguzi na hiari yake hujitenga na njia ya maumbile hayo na uongofu wa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, badala ya kuifanya sauti ya ndani ya kutafuta haki kuwa taa ya kumuongoza, chini ya ushawishi wa matamanio ya nafsi na mambo ya mazingira, huchagua njia tofauti na njia ya maumbile yake ya kiungu.

Kinachofanya utafiti huu kuwa muhimu ni kwamba kusahau au kubadili mwelekeo wa maumbile ya asili ya kiungu husababisha kubadilika kwa neema za Mwenyezi Mungu.

Tafakari mfano huu wa Qur’ani: “Watu wa Lut” walikuwa watu walioadhibiwa kwa sababu ya kufanya madhambi makubwa, miongoni mwao ikiwa ni “kulawati.” Mtume wa watu hao alikuwa Mtukufu Lut (as). Kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria, watu wa Lut, baada ya kutokukoma kufanya “madhambi makubwa”, miongoni mwao ikiwa ni “kulawati”, hatimaye walikumbwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Qur’ani Tukufu imeeleza adhabu ya watu wa Lut kuwa ni kupinduliwa kwa ardhi na kunyeshewa mawe kutoka mbinguni.

«وَأَمْطَرْنَا عَلَیْهِمْ مَطَرًا فَانْظُرْ کَیْفَ کَانَ عَاقِبَةُ الْمُجْرِمِینَ.» 

“Na tukawateremshia mvua (ya mawe); basi tazama ulikuwaje mwisho wa wahalifu.”

(A'rafi/84)

Na pia anasema:

«فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا جَعَلْنَا عَالِیَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَیْهَا حِجَارَةً مِنْ سِجِّیلٍ مَنْضُودٍ.» 

“Basi ilipo fika amri yetu tuliigeuza nchi juu chini, na tukawateremshia mvua ya changarawe za udongo mgumu ulio kamatana wa Motoni.”

(Huud/ 82)

Kwa hiyo, kwa mtazamo wa mafundisho ya kimaadili na kidini ya Uislamu, miongoni mwa madhambi ambayo yanaweza kumweka mwanadamu mbali na njia ya maumbile ya asili ya kiungu na kuandaa mazingira ya kubadilika kwa neema za Mwenyezi Mungu ni “mapenzi ya jinsia moja.”

Dhambi na kukaidi njia ya Mwenyezi Mungu huiondoa neema katika hali yake iliyokusudiwa na kugeuza “mvua ya rehema” kuwa “mawe ya adhabu”; taswira inayomwita mwanadamu kutafakari juu ya madhara ya kiroho ya dhambi, kurejea katika maumbile ya asili ya kiungu na kuomba msamaha na rehema za Mwenyezi Mungu.

Ndiyo maana nafasi ya maneno matukufu ya Amir al-Mu’minina Ali (as) katika “Dua ya Kumayl” inazidi kudhihirika:

«اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِیَ الذُّنُوبَ الَّتِی تُغَیِّرُ النِّعَمَ.»

“Ewe Mwenyezi Mungu! Nisamehe madhambi yanayobadilisha neema.”

Kwa sababu hiyo, muumini daima anapaswa, kwa ajili ya kuondolewa kwa balaa (kuokolewa kutokana na athari na madhara ya dhambi), na pia kwa ajili ya kuzuia balaa (kujikinga na kuangukia katika dhambi na kubadilika kwa neema), kumwomba Mwenyezi Mungu msamaha na rehema kwa unyenyekevu, na kuchukua hatua katika njia ya kujirekebisha.

Jibu kwa swali moja:

Ikiwa kwa mujibu wa mafundisho ya kidini, dhambi ya ushoga inahusisha adhabu ya Mwenyezi Mungu na kubadilika kwa neema za Mwenyezi Mungu, kwa nini basi wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja katika jamii za leo, hususan katika jamii za Magharibi, hawapati adhabu ya Mwenyezi Mungu, na pengine hata wanafurahia baadhi ya neema za Mwenyezi Mungu?

Jambo linalopaswa kuzingatiwa mwanzoni mwa kujibu swali hili ni kwamba adhabu iliyoahidiwa haihusiani na mafundisho ya Uislamu pekee.

Katika Waraka kwa Warumi katika Biblia imeelezwa hivi:

“Kwa hiyo Mungu aliwaacha katika tamaa zao za aibu. Hata wanawake wao walibadilisha matumizi ya asili na yale yasiyo ya asili. Vivyo hivyo, wanaume pia wakaacha matumizi ya asili ya wanawake, wakawaka kwa tamaa wao kwa wao. Wanaume wakafanya matendo ya aibu pamoja na wanaume, wakapokea ndani yao malipo yaliyostahili upotovu wao.”

(Warumi 1:26–27)

Biblia inazungumzia malipo yanayostahili upotovu wa mapenzi ya jinsia moja. Malipo hayo ni yapi?

Katika Kitabu cha Walawi, malipo hayo yametajwa hivi: “... Wala usilale na mwanamume kama ulalavyo na mwanamke, maana ni machukizo. ... Msijitie unajisi kwa mambo hayo yote, kwa maana kwa mambo hayo mataifa nitakayoyafukuza mbele yenu yamejitia unajisi. Nchi nayo imekuwa najisi; kwa hiyo nimeupatiliza uovu wake, nayo nchi imewatapika wenyeji wake. Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu...”
(Walawi 18:22, 24, 25, 26)

Kisasi na ghadhabu ya ardhi ni ile adhabu inayotokana na kutokujali maumbile ya asili ya kiungu na maumbile ya mwanadamu; adhabu hiyo hiyo ambayo Qur’ani Tukufu pia imeieleza:

«فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا جَعَلْنَا عَالِیَهَا سَافِلَهَا... .»

“Na ulipofika amri yetu, tuliifanya sehemu yake ya juu kuwa ya chini...”

(Huud/ 82)

Kwa hiyo, adhabu iliyoahidiwa haihusiani na mafundisho ya Uislamu pekee.

Jambo jingine linalopaswa kuzingatiwa katika kujibu swali hili ni kwamba; kucheleweshwa kwa adhabu ya Mwenyezi Mungu, pamoja na mtu kufurahia neema za Mwenyezi Mungu na kutobadilika kwa neema hizo, si ishara ya kuidhinishwa kwa kitendo hicho (= dhambi).

Mwenyezi Mungu Mtukufu, akizungumzia watu ambao wamezisahau amri za Mwenyezi Mungu lakini kwa sura ya nje wanaonekana kufurahia neema za Mwenyezi Mungu, anasema:

«فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُکِّرُوا بِهِ فَتَحْنَا عَلَیْهِمْ أَبْوَابَ کُلِّ شَیْءٍ حَتَّیٰ إِذَا فَرِحُوا بِمَا أُوتُوا أَخَذْنَاهُمْ بَغْتَةً فَإِذَا هُمْ مُبْلِسُونَ.» 

“Basi waliposahau yale waliyokumbushwa, tuliwafungulia milango ya kila kitu (cha neema); mpaka walipofurahia yale waliyopewa, ghafla tuliwakamata, na mara wakawa wamekata tamaa; (milango ya matumaini ikafungwa mbele yao).”

(Ana'mi/ 44)

Ndiyo maana Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) amesema:

«إِذَا رَأَیْتَ اَللَّهَ یُعْطِی عَلَی اَلْمَعَاصِی فَإِنَّ ذَلِکَ اِسْتِدْرَاجٌ مِنْهُ.»

“Ukiuona ulimwengu ukiwanawiria wenye kufanya madhambi, basi hiyo ni istidraaj ya Mwenyezi Mungu kwake; yaani kuwaangamiza hatua kwa hatua.”
(Tafsir Nuuru Thaqalain, Juzu 1, Uk: 718)

Kwa hiyo, kwa mujibu wa mafundisho ya kidini, “sunnah ya istidraaj” ni miongoni mwa sunnah na sheria za Mwenyezi Mungu. Maana yake ni kwamba ikiwa mtu amejitenga na njia ya maumbile ya asili ya kiungu, lakini wakati huohuo anaendelea kufurahia neema za Mwenyezi Mungu, anapaswa kujua kwamba yuko katika njia ya kuangamia. Na kwa hakika, hali hiyo ya starehe na kutopata adhabu kwa muda kamwe si ishara ya rehema ya Mwenyezi Mungu kwa mtu huyo mwenye kufanya dhambi.

Umuhimu wa suala hili ni mkubwa kiasi kwamba Amir al-Mu’minina Ali (as) anatukanya kuhusu ukweli huu kwa kusema:

«یَا ابْنَ آدَمَ، إِذَا رَأَیْتَ رَبَّکَ سُبْحَانَهُ یُتَابِعُ عَلَیْکَ نِعَمَهُ وَ أَنْتَ تَعْصِیهِ، فَاحْذَرْهُ.»

“Ewe mwanadam! Unapomuona Mola wako Mtukufu akiendelea kukuteremshia neema zake mfululizo, huku wewe ukimuasi, basi jihadhari naye (usije ukawa unangojea adhabu yake kali).”
[Nahjulbalagha, Hekima ya 25]

Ingawa kuna maandiko mengi kuhusu hatari ya dhambi ya ushiriki wa mapenzi ya jinsia moja, na ushahidi unaokumbusha juu ya hatari hiyo, lakini — kwa ajili ya kufupisha — tunatosheka na kiasi hiki.

Mustafa Amini

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha