Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, katika hali ya kuongezeka mashambulizi ya adui wa Kizayuni dhidi ya Lebanon, hususan baada ya kufanya mauaji mawili katika miji ya Ansar na Deir al-Zahrani kwa kuwalenga raia, maswali yameongezeka kuhusu manufaa ya kuendelea kwa mazungumzo ya viongozi wakati mvamizi akiendelea na mashambulizi yake, na kuhusu uwezo wa viongozi kufikia matokeo yatakayohifadhi mamlaka na haki za Lebanon, katika hali ya kukosekana dalili zilizo wazi za nguvu.
Karim Bqeradouni, mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Kataeb, katika mahojiano na tovuti ya habari «Al-Ahed», alisema: Lebanon inakabiliwa na hali isiyo na uwiano, kwa sababu Israel kwa upande mmoja inafanya mazungumzo, na kwa upande mwingine inaendelea na mashambulizi na mauaji ndani ya ardhi ya Lebanon. Anaona kwamba kuendelea kwa hali hii kunailazimu Lebanon kuupitia upya mwelekeo wake wa mazungumzo.
Kwa mtazamo wake, hali hii haiwezi kuendelea, kwa sababu mazungumzo yanapaswa kuambatana na kusitishwa kwa hatua za uhasama, wakati hali halisi ya uwanjani inaonesha kuendelea kwa mashambulizi.
Aliongeza kuwa: Kuendelea kwa mauaji ya Israel nchini Lebanon, wakati huo huo ikiwa inafanya mazungumzo na viongozi, kunaiweka Lebanon mbele ya hali hatari; hasa wakati mashambulizi yanafikia kuzilenga familia zote na kusababisha wanawake, wazee na watoto kuuawa kishahidi.
Bqeradouni aliieleza hali hii kuwa ni mazingira ambayo hapo awali Israel haikuwahi hata kuyatamani. Alisema: Utawala huu ulikuwa ukianzisha vita na mashambulizi, lakini wakati huo huo haujawahi kuwa katika nafasi ya kufanya mazungumzo ya kisiasa kwa namna hii. Lakini leo, kwa mujibu wa tathmini yake, Israel inamuua yeyote anayemtaka na kufanya mazungumzo na yeyote anayemtaka.
Kiongozi huyo wa zamani wa Chama cha Kataeb alisema: Hali hii inaupa utawala huo nafasi pana ya kufanya harakati za kijeshi na kisiasa kwa wakati mmoja. Akisisitiza kwamba Lebanon haiwezi kuendelea kushughulikia hali hii kana kwamba ni jambo la kawaida, aliongeza: Tunawataka viongozi waupitie upya mwelekeo wa sasa.
Kipaumbele ni usitishaji wa mapigano
Bqeradouni alisisitiza kwa kusema: Kipaumbele kinapaswa kuwa usitishaji wa mapigano na kusitishwa kwa mauaji ya raia, hususan wanawake, wazee na watoto. Anaamini kwamba kuendelea kuwalenga raia kunafanya mazungumzo yenye uwiano kuwa magumu, na kwamba njia yoyote ya kisiasa ambayo haitakomesha mashambulizi haitakuwa na uwezo wa kuilinda Lebanon na Walebanon.
Aliongeza: Kuendelea kwa hali ya sasa kwa kipindi kirefu hakutakuwa na manufaa kwa Lebanon, bali kutaongeza hasara zinazoikumba nchi na watu wake. Bqeradouni, akisisitiza kwamba; ukatili wa Israel haukomi na hauna mipaka, alionya kwamba kuendelea kwa hali hii kutaiathiri Lebanon na Walebanon na hakutakuwa na manufaa kwa nchi.
Viongozi hawana nguvu
Bqeradouni anaona sehemu muhimu ya tatizo ni viongozi, na anaamini kwamba viongozi wa Lebanon wanaingia katika mazungumzo bila kuwa na karata ya kushinda wala nguvu iliyo wazi. Mwenyekiti huyo wa zamani wa Chama cha Kataeb alisisitiza: Kuwepo kwa karata ya kushinda na msimamo mmoja wa Walebanon kungeweza kuyafanya mazungumzo yawe na uwiano zaidi, wakati mazungumzo katika hali yake ya sasa hayana uwiano.
Alihusisha ukosefu wa nguvu na kuendelea kwa mashambulizi ya Israel, na akauliza kuhusu sababu zinazomfanya mvamizi azidishe mashambulizi yake licha ya kuendelea kwa mchakato wa mazungumzo.
Maoni yako