Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Idara ya Nyumba ya Wageni wa Mazuwari katika Haram Tukufu ya Amiri wa Waumini (amani iwe juu yake) imeanza kutekeleza mpango kamili wa kufturisha Ramadhani, kwa baraka za Kiongozi wa Wachamungu, Ali ibn Abi Talib (amani iwe juu yake). Mpango huu unajumuisha kuandaa meza za futari za kila siku na kila wiki kwa mazuwari, pamoja na meza za futari nje ya haram tukufu ndani na nje ya mkoa wa Najaf Ashraf, ukihusisha taasisi za kibinadamu na makundi mbalimbali ya kijamii kutoka mikoa tofauti ya Iraq.
Athir Al-Tamimi, mkuu wa idara ya nyumba ya wageni, alisema: Mpango huu unatekelezwa kwa amri na chini ya usimamizi wa Uongozi wa Haram Tukufu ya Alawi, na meza za kwanza za futari zilifunguliwa katika Uwanja wa Bibi Zahraa (amani iwe juu yake), jirani na Haram Tukufu ya Amiri wa Waumini (amani iwe juu yake).
Aliongeza kuws: Meza hizi zitaandaliwa kila wiki kwa ajili ya kuwahudumia mazuwari wa Kiongozi wa Waumini (amani iwe juu yake), sambamba na mpango wa kila siku wa ftari unaoratibiwa ama kupitia uhifadhi wa kielektroniki au kupitia ofisi ya usambazaji wa vocha za nyumba ya wageni, pamoja na timu za simu zilizopo ndani na pembezoni mwa uwanja mtakatifu.
Al-Tamimi pia alieleza kuwa, mpango wa safari za Ramadhani utajumuisha nyumba za wazee, taasisi za hisani na kijamii, pamoja na makundi ya wahitaji katika mikoa kadhaa ya nchi; aidha utawajumuisha wanafunzi wanaoishi katika mabweni. Mpango huu unatekelezwa katika muktadha wa misaada ya kibinadamu na kijamii ambayo Haram tukufu ya Imam Ali (as) daima huipa kipaumbele ndani ya Mwezi wa Ramadhani.
Inafaa kutajwa kuwa, Idara ya Mazuwari inaendelea kusambaza milo ya futari kwa familia zenye uhitaji katika maeneo yenye hali ngumu, na sambamba na hilo inawasaidia maelfu ya mayatima na wahitaji kupitia mpango wake wa Ramadhani.
Hatua hizi ni dhihirisho la roho ya kujitolea, ukarimu na mshikamano wa kijamii ambao Haram Tukufu ya Alawi ni kielelezo chake, na zinaendelezwa katika utekelezaji wa ujumbe wake wa kibinadamu na kidini katika kuwahudumia mazuwari na jamii kwa ujumla.
Maoni yako