Jumatano 11 Februari 2026 - 00:40
Wananchi kushiriki katika tarehe 22 Bahman ni tangazo la kusimama imara pamoja na Mapinduzi na sababu ya kuwakatisha tamaa maadui

Hawza/ Ayatullah Shabzendeh-Dar, huku akisisitiza umuhimu maradufu wa maandamano ya Yawmullah (Siku ya Mwenyezi Mungu) ya tarehe 22 Bahman katika mazingira ya sasa, alieleza kuwa ushiriki mpana wa wananchi ni ishara ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema kubwa ya Mapinduzi ya Kiislamu na ujumbe wazi kwa maadui kwamba taifa la Iran linasimama imara pamoja na mfumo wa dola, Mapinduzi na maadili ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Shabzendeh-Dar katika mazungumzo na Shirika la Habari la Hawza, huku akirejelea kuwadia kwa Yawmullah ya tarehe 22 Bahman, alisema: Tarehe 22 Bahman, siku ya ushindi wa Mapinduzi matukufu ya Kiislamu, ni matunda ya harakati iliyodumu kwa muda wa miaka kumi na tano tangu mwanzo wake chini ya uongozi wa Imam Khomeini (r.a), ambayo iliendelea katika hali na vipindi mbalimbali kwa gharama na juhudi nyingi za wananchi wapendwa na wanazuoni wakubwa wa dini, na kwa fadhila na rehema za Mwenyezi Mungu ikafikia ushindi.

Aliongeza kuwa: Katika siku hii kubwa, mfumo wa ubeberu na utawala wa kitwaghuti, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, uliondolewa na kuanguka, na mfumo wa kifalme wa miaka 2500 ukaporomoka, na mazingira ya kusimamishwa kwa mfumo wa Kiislamu yakapatikana.

Ayatullah Shabzendeh-Dar aliendelea kusema: Baada ya ushindi wa Mapinduzi pia, wananchi kwa ushiriki wa kipekee na kura iliyokaribia asilimia mia moja waliipigia kura Jamhuri ya Kiislamu. Katika kipindi cha miaka 47 tangia ushindi huo mkubwa, taifa la Iran daima limekuwa likiadhimisha siku hii kwa kushiriki kwa wingi katika maandamano ya tarehe 22 Bahman na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hii kubwa ya Kiungu.

Katibu wa Baraza Kuu la Hawza za Kielimu alisisitiza: Leo pia kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa neema hii kubwa ya Kiungu na kwa uangalizi na fadhila za Mawalii wa Mwenyezi Mungu, hususan Baqiyyatullah al-Aʿdham (a.f), ni jambo la lazima sana na muhimu.

Alibainisha kuwa: Ushiriki katika maandamano ya tarehe 22 Bahman, katika mazingira ya sasa, una umuhimu maradufu; hasa kutokana na hali tunazokabiliana nazo leo. Kama alivyosema Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, ikiwa maadui wa Uislamu na wanaoupinga mfumo huu wenye baraka pamoja na nchi yetu pendwa — ambao wanakusudia kuidhuru na hata kuigawa — watakata tamaa ya kufikia malengo yao ya kishetani, kwa kawaida madhara na matatizo wanayoyasababisha yatapungua.

Ayatullah Shabzendeh-Dar alisisitiza: Hivyo basi, ni wajibu kwa wote — wakiwemo wananchi wapendwa wa matabaka mbalimbali, wanaume na wanawake, na hasa wanazuoni wakubwa wa dini na wanafunzi wa elimu ya dini ambao wamekuwa na nafasi kubwa katika kuasisiwa na kuendelea kwa Mapinduzi haya — kushiriki katika maandamano na mikusanyiko inayofanyika kwa mnasaba huu, ili kwa hakika kutuma ujumbe wazi kwa ulimwengu, maadui, madhalimu na wenye nguvu za mabavu duniani.

Katibu wa Baraza Kuu la Hawza za Kielimu aliongeza: Ushiriki huu utatangaza kwamba; sisi tumesimama imara pamoja na mfumo wa dola, Mapinduzi na maadili yetu, na kwamba matatizo na mashinikizo yanayoletwa na maadui hayatatuchosha, kutukatisha tamaa wala kutuondoa katika uwanja wa mapambano. Tamko hili ni ujumbe muhimu sana unaowasilishwa kwa ulimwengu kupitia uwepo huu wa wananchi, na kwa upande mwingine ni aina ya kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Mwalimu huyu wa Hawza aliendelea kusema: Miongoni mwa athari nyingine za ushiriki huu ni kwamba; viongozi wa nchi wanapouona msaada wa wananchi wanapata matumaini zaidi na wanaweza kutekeleza majukumu yao na kufanya khidma kwa ari kubwa zaidi. Vilevile, vikosi vya ulinzi vya nchi ambavyo, tunamshukuru Mwenyezi Mungu, vimeonesha nguvu na uaminifu wao katika nyakati mbalimbali, vinapata hamasa na mshikamano zaidi vinapoona uungwaji mkono wa wananchi.

Ayatullah Shabzendeh-Dar alisisitiza pia: Wananchi, viongozi na vikosi vya ulinzi wanapokuwa pamoja na kusaidiana, sauti moja ya umoja itasikika kutoka katika nchi hii; na bila shaka maadui watakata tamaa, na huenda wakaacha njama na uadui wao au kuupunguza kwa kiwango kikubwa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha