Jumatatu 26 Januari 2026 - 23:12
Jaribio lolote la kuivamia heshima ya Wilaya litajibiwa kwa tufani ya hasira ya Umma wa Kiislamu

Hawza/ Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlul-Bayt wa Uturuki, huku ikitoa onyo kwa Marekani na Israel, imesisitiza: Jaribio lolote la kuvunja au kuvamia heshima ya Wilaya na Uongozi ni mstari mwekundu usiovukwa kabisa, na litakabiliwa na tufani ya hasira takatifu ya Umma wa Kiislamu, ambayo itakuwa na matokeo ya uharibifu mkubwa kwa wavamizi.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlul-Bayt wa Uturuki mjini Istanbul, kwa kutoa tamko rasmi, huku ikisisitiza kwamba bendera ya dhulma na ubeberu ipo mikononi mwa Marekani na utawala wa Kizayuni unaonyakua ardhi, imeitaja kambi ya Muqawama, chini ya uongozi wa hekima wa Imam Khamenei, kuwa ni kinara wa uhalisia wa haki na utekelezaji wa uadilifu duniani.

Wanazuoni wa Ahlul-Bayt wa Uturuki katika tamko hili pia wamezionya nguvu za kibeberu kwamba vitakatifu vya Kiislamu na nafasi tukufu ya Wilaya ni mstari mwekundu kamili na wa msingi, na aina yoyote ya kukosa heshima kwa eneo hili takatifu italeta matokeo ya uharibifu mkubwa kwa wavamizi.

Matini kamili ya tamko hilo ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

Leo, ubinadamu kwa ujumla, na hasa ulimwengu wa Kiislamu, unapitia moja ya nyakati nyeti zaidi katika historia yake. Mipaka kati ya haki na batili imejitokeza kwa uwazi usio na kifani, si tu katika Mashariki ya Kati bali katika pembe zote za dunia, na kambi mbili zimejipanga uso kwa uso.

Kwa kila mwenye akili na dhamiri iliyo hai, ni dhahiri kwamba bendera ya dhulma na uistikbari iko mikononi mwa Shetani Mkubwa, yaani Marekani, pamoja na zao lake haramu — utawala wa Kizayuni unaonyakua ardhi. Kwa upande wa pili, kambi tukufu ya Muqawama, chini ya uongozi na amri ya hekima ya Imam Khamenei, imesimama kama kinara wa kambi ya haki kwa ajili ya kutimiza uadilifu na kuwaokoa wanyonge duniani.

Katika kipindi hiki cha hatima, kusimama dhidi ya madhalimu na kuwasaidia waliodhulumiwa ni wajibu wa kisheria na wa kibinadamu kwa watu wote huru wa dunia.

Kwa njia hii, kwa mara nyingine tena tunapaza sauti yetu tukitangaza kwamba kuanzia Palestina hadi Yemen, kuanzia Lebanon na Syria hadi Myanmar na Venezuela, tutabaki kuwa wasaidizi na wasuhuba wa waliodhulumiwa duniani kote.

Kwa uwazi kamili, tunazionya nguvu za kibeberu kwamba vitakatifu vya Kiislamu na nafasi tukufu ya Wilaya na uongozi wa kidini, ambao leo bendera yake inabebwa na Mtukufu Ayatullah al-‘Udhma Imam Khamenei, ni mstari wetu mwekundu wa mwisho na wa msingi. Ikiwa mabeberu wana chembe yoyote ya wasiwasi juu ya kuendelea kuwepo kwao, basi waondoe hata wazo la kuvamia heshima hii takatifu kutoka katika akili zao; vinginevyo watakabiliwa na tufani ya hasira takatifu ambayo itawaletea matokeo ya uharibifu mkubwa na yasiyoweza kufikiriwa.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atujalie ushindi wa mwisho wa kambi ya haki na umoja wa neno la Umma wa Kiislamu.

Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlul-Bayt wa Uturuki – Istanbul

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha