Jumamosi 24 Januari 2026 - 00:00
Waziri wa Ulinzi wa Pakistan: Katika hali yeyote tutasimama imara upande wa Iran

Hawza/ Khawaja Muhammad Asif, Waziri wa Ulinzi wa Pakistan, katika kikao chake na Reza Amiri Moghaddam, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Islamabad, walijadili na kubadilishana mawazo kuhusu maendeleo ya kikanda na upanuzi wa uhusiano wa pande mbili.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Khawaja Muhammad Asif, Waziri wa Ulinzi wa Pakistan, katika mkutano wake na Reza Amiri Moghaddam, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Islamabad, walijadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu mabadiliko ya kikanda na kuimarisha uhusiano wa pande mbili.

Waziri wa Ulinzi wa Pakistan, huku akisisitiza uhusiano wa kina, wa kihistoria na wa kindugu kati ya Pakistan na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alitangaza kuwa Islamabad katika hali zote na kwa msimamo thabiti itasimama upande wa Iran.

Akirejelea mafungamano ya kina ya kijamii, kitamaduni na kihistoria kati ya nchi hizo mbili, alisema: wananchi na serikali ya Pakistan daima wamesimama upande wa taifa la Iran katika nyakati ngumu, na wana imani kamili na busara pamoja na uwezo wa wananchi na viongozi wa Iran katika kushinda changamoto.

Katika mkutano huu, pande zote mbili zilisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa pande mbili kwa misingi ya heshima ya pande zote, maadili ya pamoja na ushirikiano wa kikanda.

Balozi wa Iran pia, huku akitoa shukrani kwa uungaji mkono endelevu wa serikali na wananchi wa Pakistan, alisifu msimamo wa kimsingi na wa kirafiki wa Islamabad kuielekea Iran.

Chanzo: ble.ir/PakistanStudies

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha