Jumanne 30 Desemba 2025 - 20:55
Brazil nayo yaungana na jumuiya ya wanaohifadhi Qur’ani

Hawza/ Kozi ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu kwa watoto Waislamu imeandaliwa katika mji wa São Paulo, Brazil, kwa lengo la kuimarisha utambulisho wa Kiislamu na maadili ya kielimu miongoni mwa vijana.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kozi hii iliyoanza takribani mwezi mmoja uliopita, imeandaliwa na Kituo cha Kimataifa cha Kiislamu kwa lengo la kueneza moyo wa kupenda amani nchini Brazil na Amerika ya Kusini, na kwa bahati nzuri imepokelewa vyema na familia za Kiislamu. Madarasa haya, kulingana na ratiba, hufanyika mara kadhaa kwa wiki na yanatoa mazingira ya kielimu na kijamii yaliyoandaliwa kwa watoto na vijana.

Mtaala wa programu unajumuisha kuhifadhi Qur’ani, kanuni za tajwidi, na ufafanuzi wa hadithi arobaini zilizochaguliwa kutoka kwa Mtume Mtukufu (Rehema na Amani zimshukie yeye na Aali zake), pamoja na masomo ya itikadi, fiqhi, maadili na maarifa ya jumla ya kidini. Katika programu hii, shughuli za kielimu zimeandaliwa kwa watu wenye umri tofauti ili kuhamasisha ushiriki katika masuala ya kidini.

Idadi ya wanazuoni na wahubiri mashuhuri wa Kiislamu nchini Brazil, chini ya usimamizi wa Abdulhamid Mutawalli, mkuu wa kituo hicho, walitoa hotuba katika hafla ya ufunguzi. Programu hii inatarajiwa kuendelea hadi mwisho wa mwezi wa Januari na itahitimishwa kwa kuandaliwa hafla ya kuwapongeza washiriki bora.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha